habari wadau,
kama mtakumbuka vizuri,mwaka 2010 wanafunzi wengi wa vyuo vikuu nchini walishindwa kushiriki katika uchaguzi mkuu wa wabunge na raisi kutokan na wanafunzi hao kujiandikisha wakiwa vyuoni ili hali wakati wa uchaguzi vyuo vingi vinakuwa bado vimefungwa.
Hivyo basi,kwakuwa zoezi la kuboresha daftari la wapiga kura ndio limekaribia kuanza,ni vyema hatua zikachukuliwa mapema kwa kuweka utaratibu maalumu utakaowawezesha wanafunzi hao kujiandikisha na kisha kupiga kura wakati ukifika bila kikwazo chochote.
Ukawa,vijana ndio mtaji wetu,hivyo basi, hatuna budi kuibeba hii agenda mapema ili vijana hawa mwakani wasipoteze haki yao ya kupiga kura.
Mimi naomba nimalizie kwa kuongezea katika kauli mbiu yetu ya ukawa kama ifuatavyo;
"ukawa tumaini letu na tumaini la ukawa ni vijana wetu".