Ukatili

Calamity

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2013
Posts
856
Reaction score
47
Jamani wakubwa nimeshuhudia mambo haya yakifanyika

jana usiku wa tarehe 14-08-214 saa 2.00 baba mmoja tena mtumishi wa umma ambaye ni dereva wa gari la SU mali ya wizara ya kilimo na mifugo hapa jijini mwanza anayeishi nyakato eneo la Mahango karibu na (fance ya gachuma)
Baada ya kurudi kutoka kazini usiku akakuta familia yake iko salama ,ndpo akamwita mtoto wake wa kiume aitwaye Amos umri(12-13) akamuuliza vipi wewe ulienda shule ,ndiyo baba...mtoto alijibu tena baba akasema nimekununulia soksi za shule ,lakini leteni kwanza zile ,mtoto akamjibu si nilikwambia zilipotea? baba bila kujali ndipo akaanza kumshushia kipigo cha mbwa mwizi karibia nusu saa bila kujali anapiga sehemu gani za mwii kwa kutumia mbanio wa sufulia majirani walikuwa wanachungulia kupitia dirishani.

Hadi kuamkia asubuhi mtoto hakuweza kwenda shule maaana anatapika damu mwili umejaa majeraha.

Nayule mama aliyeko sio mama yake wa kumzaa niwakambo

Jamani kumbe sisi wazazi ndio tunao ongoza kwa kufanyia watoto weu ukatili nilitamai kama nigekuwa na namba za police nigewapigia wakaja shuhudia yule mtoto.
 
Roho imeniuma jamani…!!!! Ningekua mm nimeshuhudia hilo tukio,ningeingilia nisingeweza kuangalia na kunyamaza,mtoto anauma bhana,asikwambie mtu…!!
 
kwanini msiende ripoti vyombo husika, huyo mzee mfikisheni vyombo vya sheria. Hapa haisaidii..
 

Dah... Pole kwa mtoto, haya namba za PLAN INTERNATIONAL hizi hapa.

Please do the needful kunusuru maisha ya mtoto...

028 2505064
 

We nae ni tatizo.
kwanini usiende police we unakuja kureport jamiiforum, pale kuna kituo cha mwatex kama bado hawajahama ingekimbia fasta wakamkamata.
Pole yake dogo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…