Dr PL
JF-Expert Member
- Sep 13, 2024
- 558
- 837
Huu ukatili haufai katika jamii yetu, mtoto kama huyu kupigwa makofi kiasi hicho sio sawa.
Sijui imetokea wapi na lini lakini kwa kweli haifai wala tusikubali ukatili kama huu.
Taarifa hii ni ya miaka sita iliyopita kutoka nchini Afrika ya kusini ambapo Mfanyakazi mmoja wa shule ya chekechea anadaiwa pia kumtusi msichana mdogo kwa kumtukana na kumzomea kwa sauti kali akisema: “Kwa nini unatapika? Kwa nini?”
Polisi wamemkamata mwanamke mwenye umri wa miaka 40 kuhusiana na tukio hilo, baada ya video iliyorekodiwa mwezi uliopita katika shule moja ya chekechea huko Carletonville, Afrika Kusini kuibuka.
Katika video hiyo, mwanamke huyo anaonekana akirusha karatasi ya tishu mezani na kumtaka mtoto huyo aliyekuwa mgonjwa kujifuta usoni.
Baadaye anaanza kumchapa kichwani mara kadhaa huku mtoto akilia kwa uchungu.
Anasikika akimzomea mtoto akisema: “Niambie, kwa nini unatapika? Ni raha kutapika?”
Baada ya video hiyo kusambaa mitandaoni, wazazi wengi walichukua hatua ya kuwaondoa watoto wao katika shule hiyo ya chekechea.
Mzazi mmoja, ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema:
“Nilipomweleza mkuu wa shule kuhusu hili, aliniambia kuwa binti yangu ni mtu wa hisia sana na kwamba ninareact kupita kiasi.”
Mzazi mwingine alieleza:
“Nimeshtushwa na nimekasirishwa. Hii ni moja ya shule za chekechea bora zaidi. Watoto wa polisi, maofisa wa juu, wanasheria na walimu husoma hapa.”
Mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa tena mahakamani Jumanne, Mei 7.
Msemaji wa Huduma ya Polisi ya Afrika Kusini alisema:
“Polisi wanathibitisha kuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 40 alikamatwa wiki iliyopita na kufikishwa mahakamani tarehe 28 Machi 2019 katika Mahakama ya Oberholzer, Carletonville, kwa kosa la kumshambulia mtoto mdogo.”
"Mwanamke huyo aliachiwa kwa dhamana na anatarajiwa kurejea mahakamani Mei 7, 2019, huku uchunguzi ukiendelea."
"Kwa kuwa mchakato wa mahakama umeanza na uchunguzi bado unaendelea, polisi hawawezi kutoa taarifa zaidi kwa sasa."
"Hata hivyo, uongozi wa polisi umelaani vikali tukio hilo pamoja na usambazaji usio wa kiheshima wa video hizo mitandaoni."
"Wakati huohuo, uchunguzi wa uhalifu wowote dhidi ya watoto, wanawake na makundi mengine yaliyo hatarini unaendelea kupewa kipaumbele na Jeshi la Polisi la Afrika Kusini."
"Kesi hii inashughulikiwa kwa uzito ili kuhakikisha haki inatendeka."