Kirchhoff
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,618
- 8,289
Nimeamka asubuhi mwenye mawazo sana. Jana jioni kabla ya kula, mke wangu alinionyesha video ya yaliyojiri Burundi (alikuwa kapika kitoweo pendwa wengine mnakiita "kitimoto", "mbuzi katoliki"n.k). kabla hajanionyesha aliniuliza kama nikiona picha mbaya naweza kula nyama, nikamwambia "hazintishi". Ndipo alipponionyesha video ambayo inanifanya niandike Uzi Huu na kutoa tafakari iliyotokana na mawazo niliyoamka nayo. Anyway Nilikandamiza kitoweo kama kawaida japo kidogo kwa majonzi.
Hadi sasa nimehitimisha kuwa:
"Kila binadamu anaweza kufanya ukatili endapo muda na mahali vinaruhusu."
Je Ushawahi kuwaza au kushuhudia matokeo ya yafuatayo:? ungefanyaje?
1. Ukimfumania mwenza wako au hatu aliyochukua mtu aliyefumania,
2. Ukidhulumiwa jasho lako, watu waliodhulumiwa
3.
4. ongezea nyingine, nisiwachoshe
Mara nyingi tumewaza Ukatili na mengine yanayofanana na hayo ila Muda/ mahali haukuruhusu kufanya ukatili tuliouwaza. Neema ya Mungu ilituepusha (kwa wale wanaoamini). Kwa wale waliopata nafasi (muda na mahali) waliweza kwa namna moja au nyingine kutekeleza ukatili walioufikiri.
Kanisa Moja Takatifu Katoliki la Mitume mwaka huu linaadhimisha "Mwaka Wa Huruma ya Mungu."
Tuungane nalo kuomba huruma ya Mungu iwe nasi, tuwahurumie na kuwasamehe waliotukosea, ili Mungu Mwenye Enzi Atuhurumie na Kutusamehe.
Kwa Jina La Baba Na La Mwana Na La Roho Mtakatifu. Amina.