Ukarabati wa Hospitali Halmashauri ya wilaya Bagamoyo washika kasi

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
794
501
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Willaya ya Bagamoyo Bw. Shauri Selenda, tarehe 09 Mei 2024, ametembelea na kukagua Mradi wa Ukarabati wa Hospital ya Wilaya ya Bagamoyo.

Ukarabati huo utafanyika kwa awamu ambapo awamu ya kwanza majengo yafuatayo jengo la Mama na Mtoto pamoja na Lishe, jengo la Watumishi, jengo la wodi ya wagonjwa binafsi, jengo la kuhifadhia madawa, na Jengo la kuhifadhia Maiti.

Akiwa Hospitalini hapo Mkurugenzi huyo amewataka wasimamizi na mafundi wa mradi huo kufanya kazi kwa juhudi na kuhakikisha ujenzi huo unafuata taratibu zote zilizowekwa zinazosimamia ujenzi huo ili kupata majengo yaliyobora zaidi, "Nawaagiza wasimamizi wa Mradi kusimamia kwa umakini mradi huu kwa kushirikiana na mafundi, lengo letu ni kupata majengo yenye ubora unaotakiwa ili wananchi waje kupata huduma bora kwenye mazingira mazuri".

Ukarabati wa Hospitali hiyo unafanyika ikiwa sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita ya kuboresha miundombinu ya Huduma za Afya Nchini ambapo Serikali imetoa takribani milioni 900 kwa ajili ya ukarabati huo.

20240509_134402_InSave_0.jpg
 
Na ikarabatiwe tu, bado kidogo wananchi wakate tamaa kudhani mji wao kwa kuwa ni wa kimakumbusho, pengine hata hospitali yao inapaswa iwe mifano ya majengo ya makumbusho
 
Back
Top Bottom