Ukale na Usasa katika Mapenzi

Ukale na Usasa katika Mapenzi

Joined
Jul 26, 2015
Posts
49
Reaction score
30
Wenyewe walio wajuvi wa mambo hayo waliamua kuacha wazi mlango wa maana halisi ya neno Mapenzi.

Kwa maana hyo kila mmoja akatafsiri Mapenzi ajuavyo.

Leo imekuwa kawaida kujikabidhi kwa Mwanaume bila ndoa , na katika jamii ukapewa cheo cha Mume au Mke halali wa Muhusika.

Uzamani umeonekana hauna maana,Kwani wazee walikuwa wakiutazama mwenendo wa kijana na kujiridhisha aina ya mwenza amfaae.

Walikutana,kujadili na hatimae kijana kushirikishwa katika hatua za mwisho katika ndoa.

Mambo yalinyooka,kizazi kikalindwa na hata heshima ya Familia husika ikalindwa kwa nguvu zote.

Njoo Leo katika usasa mambo ni vurugu tafrani.Kila mmoja anasauti kwa mwenzake,hajulikani nani baba nani Mama.

Fedha imewekwa mbele,mwenye kazi ndio muoaji,Mkaa uchi ndo mstaarabu katika Wanawake.

Kwangu nawatazama wazee kama Nuru,kwani walijikita sana katika Busara kuliko hisia pekee.

Walitazama yajayo katika mustakbali wa maisha ya Wahusika kwa kila mmoja kuhamasishwa kuwa sehemu ya mwenzake.

Leo mnaoana kwa kuviziana nani atatangulia kufa nani atabaki na Mali.

Kuna haja sasa kurejea nyuma na kusema Uzamani una maana,na ikibidi kuzidi kuupigia chepuo katika swala zima la Mapenzi na Uhusiano kwa ujumla.

Makungwi wenye umri wanathamani tu wakati wa binti kuolewa,tofauti na enzi hizo ambapo walitumika pindi tu kijana anapoanza kuonesha dalili za kupevuka.

Hatujachelewa na wala tusione aibu katika kujenga na kuhamasisha maadili mema katika jamii yetu.

Hatutokuwa wa kwanza mini koala,Kwani hata watu wa kada ya Afya sasa wamelazimika kuzitambua na kuzipitisha Tiba mbadala kama sehemu ya Tiba kwa Mwanadamu hata wakaweka kitengo na kozi maalum.

Tuanze sasa

Kalamu na Karatasi

(Chanzo cha Maarifa)
 
Mambo yamebadilika sana,ckuizi mzee akijadili ndoa ya mtu wengine husem mchawi...
 
Mada za jioni hizi wajameni,watu tuko kwenye ujenzi wa taifa.
 
Wanasema hakuna jipya chini ya jua,vyote vinavyotokea vilikuwepo... yawezekana hata huu usasa ulishawahi kuwepo huko nyuma
 
Back
Top Bottom