Msamiati
R I P
- Mar 6, 2011
- 1,063
- 697
Mimi sio mfatiliaji wa siasa kabisa, lakini leo wakati natizama bunge kuna jambo limenisikitisha sana. Kwanza nilimuona dada mmoja akilalamika kuwa askari wanaua wananchi wanao sogelea kandokando ya mgodi kwa ajili ya kuokota mabaki ya mawe, yule dada aliongea kwa uchungu mpaka akawa anataka kulia. Kisha mchangiaji aliefata mzee mmoja hivi mimi siwajui majina, akasema ,"watu wengine kwenye makabila yao hata wakifa kuku ni msiba mkuubwa". Mimi nimechukia sana na kama ningekuwa dodoma leo ningelala polisi, sikujua kama kuna mizee ------- kama lile, inawezekanaje watu wanakufa wewe ukasema kuku! kuku yeye na mke wake na familia yake yote mshenzi kabisa na azidi kulaanika tumbo lishuke mpaka alibebe na toroli.