Wakala wa Yaya Toure Dimitri Seluk amedai kuwa mchezaji huyo ataondoka katika klabu ya Manchester city baada ya Pep Guardiola kuchukua jukumu la kuifundisha kablu hiyo.
Toure na Guardiola walifanya kazi pamoja wakiwa Barcelona kati ya mwaka 2008 na 2010 kabla ya mchezaji huyo kuhamia England.
Juzi Manchester City ilithibitisha kutua kwa kocha Guardiola ambaye ataanza rasmi kuifundisha timu hiyo kuanzia msimu ujao wa 2016/17.Mara baada ya kutangazwa kwa ujio wa kocha huyo wakala wa Yaya Toure Dimitri Seluk aliliambia gazeti la The Sun "Nafikiri Yaya ataondoka katika klabu hii. Lakini ni matumaini yangu kuwa kabla ya kuondoka ataisaidia timu kutwaa ubingwa wa ligi na makombe mengine".
"Hakuna sababu ya kuuliza kama Pep anampenda au la, ni kawaida katika maisha. Najua Pep atampigia simu Yaya na kuzungumza naye ili kujua kama yupo kwenye mipango yake au la".Yaya atafungua milango sasa kwa timu mbalimbali za uingereza na hispania zilizokuwa zinamuwinda tokea awali ili kunasa saini yake kwa msimu ujao.
SOURCE: DAR ES SALAAM WIRE BLOG