Ujinga wa Mwafrika kupenda kujiita majina ya nje ya bara lao la Africa

Sasa kumbe umejua kwamba umeyapokea kwa propaganda... Kwa nn usiyakatae?!
Ukishaitwa David.. Inkuongezea nn?!
ivi akati unapewa hilo jina ulikuwa unafahamu.

umekuja pata ufahamu lini kwamba hayo majina ni ya kutoka nje?, baada ya hapo unafahamu mlolongo wa kubadiri jina ulivyo.

kubwa zaidi wengi hawafahamu hata makabila yao (mila na desturi) unaenda jipa jina gani toka katika kabila lako.
 
Wanaita hayo majina wakidhani watoto wao watakuwa kama hao wenye hayo majina. Mfano, mtu anamwita mwanae Jaden utadhani atakuwa kama Jaden Smith hahaha. Wanangu wote nimewapa majina ya kiasili regardless of their meanings.
Mmoja anaitwa Nyabasi Nyamuhanga Chacha, mwingine anaitwa Rehema Nyamuhanga Chacha.
Hila wanawake wengi ndio wenye ulimbukeni huu
 
K
Mbona unajitekenya na kucheka mwenyewe mkuu..?? Huoni hata wewe hilo neno "BECAUSE" hapo kwenye point yako, limeonesha unatukuza kizungu chao kuliko kiswahili..??

Acheni wivu wa kijinga bana. Naamini hata wewe ungepewa nafasi ujichagulie jina WAKATI UNAJITAMBUA, labda usingejiita Mwasakafyuka, Ndahani, Mipumbutu.
Kwa hiyo inabidi tuwatukuze wazungu ? Basi tufuate mila zao za kishoga , au unasemaje ?
 
Wanaita hayo majina wakidhani watoto wao watakuwa kama hao wenye hayo majina. Mfano, mtu anamwita mwanae Jaden utadhani atakuwa kama Jaden Smith hahaha. Wanangu wote nimewapa majina ya kiasili regardless of their meanings.
Mmoja anaitwa Nyabasi Nyamuhanga Chacha, mwingine anaitwa Rehema Nyamuhanga Chacha.
Wangu mmoja nimempa ng'itimonto chacha mwita
 
Kila mtu ana uhuru wa kuchagua jina analopenda kumpa mwanae. Bado sijaona oja yako hapo, siwezi mwita mwanagu tabu,shida,sikujua, chausiku..n.k kisa uenzi uafrika
 
Ukimaliza hiyo Sheria masufuria myatupe mrejee kwenye vyungu mpikie, na Computer na simu muache kutumia mjini mje na punda na mjifunike na ngozi mkitembea....

Kuna Watu akili zao zipo makalioni hawajui wanaenda wapi na hawajui walipotoka yaani wamekuwa wapumbavu pumbavu tu.

Yaani akili zao zzinawaza miaka mia nyuma. ni watu hatari sana nyie maana ndio Ajenda ya Boko Haram hiyo hawataki elimu ya kimagharibi... huku bidhaa zote wanatumia za kimagharibi..
Mkuu nakuunga mkono mia kwa mia.wt hawazi vitu vya maana bali vya maana wanataka viwe negative
 
ivi akati unapewa hilo jina ulikuwa unafahamu.

umekuja pata ufahamu lini kwamba hayo majina ni ya kutoka nje?, baada ya hapo unafahamu mlolongo wa kubadiri jina ulivyo.

kubwa zaidi wengi hawafahamu hata makabila yao (mila na desturi) unaenda jipa jina gani toka katika kabila lako.
Tangu mwanzo..hii ipo kwenye ukoo. Tunaheshimu ancestry... Huwezi kuheshimiwa kama utasahau unatoka wapi na wewe ni nani.

Unaweza kupewa unapokuwa na akili timamu unaruhusiwa kubadili jina. Ukiona wewe ni mzalendo na unajitambua unabadilisha.

Majina ni badge ya utaifa. Wachina, wahindi, wamexico woote wanatunza asili zao.. Hao waingereza wanaheshimu ya kwao.. Sisi tunajisahau..tunajiaminisha wao ni bora zaidi yetu..

Ukishakuwa na mentality hiyo huwezi kujitetea tena mbele yao.. Unadharaulika unaonekana unajipendekeza... Waafrika hawakuthamini wala kukuheshimu.. Na hao wazungu hawakurhamini wala kukuheshimu.. Unabaki yatima.

Heshimu utamaduni.. Wako. Bila hivyo tutakuwa taifa la waenda kama Bendera... Maana Tamaduni na miiko ndiyo nanga za utaifa.. Mkianza kuzipuuza mmepotea.. Mnakuwa.kama kikundi cha wehu na walevi kinachotembea kuelekea kusikojulikana... Kila takataka ( tamaduni za kigeni) mtazipokea bila kuhoji maana hamna msingi wa kuzihoji.
 
Napendekeza hapa kwetu Tanzania itungwe sheria lazima mtoto akizaliwa apewe Jina lenye la kiafrica au kibantu, nawapongeza sana Wanyakyusa sana kwa kudumisha mila na desturi zao

Mimi langu Midumare Iwato Ngatuni Nabila midimito Mbasha,

Karibuni sana ndugu zangu wenyekuchangia vema ili tuweze kuokoa kizazi chetu kiondokane na utamaduni wang'ambo
Hili suala mtu ikimwita 'JIWE'/MWAMBA badala ya PETRO atakupiga hata jiwe.
Japan, China, Korea, India na kwingineko hawana ujinga wetu.
Ukimuita mtoto ZAWADI atakasirika...sasa muite 'GIFT' atakenua.
Muite 'Kicheko' badala la Isaac atakukunjia sura.
Muite Furaha/ Neema/ Baraka hatokenua jino, sasa muite Grace, Blessings na uzungu mwingine ndo atafurahi.
Africa ukoloni mamboleo umetamalaki....unapinga mila na tamaduni za nje huku unaitwa jina la John, Brown , Harry, Ben, Julius ( ni mifano tu and sorry kwa wenye haya majina , no offense intended)
 
Utakuta mndali, mhehe mnyiha, mfipa, mkinga mzaramo, mchaga, muha, msukuma mmakonde nk, wanaitwa Mariaclara, cleopatra, patricia, marcus, antonieta, agustus,
Kuna wato siku hizi ukisikia mama yake anamuita unadhani atakuja mzungu kumbe ni mtu mweusi kuliko wa Sudani kusini. copy and paste itapoteza hata koo zetu kama Laizer, Pallangyo, Masanja, Kimaro, Mrema, Mwakasege, Rutashobya , Rugemalila, Mwita n.k
 
Napendekeza hapa kwetu Tanzania itungwe sheria lazima mtoto akizaliwa apewe Jina lenye la kiafrica au kibantu, nawapongeza sana Wanyakyusa sana kwa kudumisha mila na desturi zao

Mimi langu Midumare Iwato Ngatuni Nabila midimito Mbasha,

Karibuni sana ndugu zangu wenyekuchangia vema ili tuweze kuokoa kizazi chetu kiondokane na utamaduni wang'ambo
Hii ni dalili mojawapo ya vyuma kukaza, sioni kama kuna tatizo lolote kwa kuwa jina halina uhusiano wowote na maendeleo ya binadamu,

Nafikiri in bora tujadili jinsi gani bei ya grisi itashuka ili maisha yaendelee.
 
K
Kwa hiyo inabidi tuwatukuze wazungu ? Basi tufuate mila zao za kishoga , au unasemaje ?
Ukitaka kumkomboa mtu mweusi katika nyanja zote lazima uanze na fikra zake.. Ila hapa mtabishana kwakuwa tunakubali kutokukubaliana.
 
Ita watoto wako majina unatyotaka na ukiweza shawishi ukoo wako na si vinginevyo.Suala muhimu ni maana ya jina tu haijalishi asili ya jina....alafu mbona elimu yao umepokea na teknolojia unatumia bila kusahau hata vyandarua mmepewa...hahahahhahh
 
Tangu mwanzo..hii ipo kwenye ukoo. Tunaheshimu ancestry... Huwezi kuheshimiwa kama utasahau unatoka wapi na wewe ni nani.

Unaweza kupewa unapokuwa na akili timamu unaruhusiwa kubadili jina. Ukiona wewe ni mzalendo na unajitambua unabadilisha.

Majina ni badge ya utaifa. Wachina, wahindi, wamexico woote wanatunza asili zao.. Hao waingereza wanaheshimu ya kwao.. Sisi tunajisahau..tunajiaminisha wao ni bora zaidi yetu..

Ukishakuwa na mentality hiyo huwezi kujitetea tena mbele yao.. Unadharaulika unaonekana unajipendekeza... Waafrika hawakuthamini wala kukuheshimu.. Na hao wazungu hawakurhamini wala kukuheshimu.. Unabaki yatima.

Heshimu utamaduni.. Wako. Bila hivyo tutakuwa taifa la waenda kama Bendera... Maana Tamaduni na miiko ndiyo nanga za utaifa.. Mkianza kuzipuuza mmepotea.. Mnakuwa.kama kikundi cha wehu na walevi kinachotembea kuelekea kusikojulikana... Kila takataka ( tamaduni za kigeni) mtazipokea bila kuhoji maana hamna msingi wa kuzihoji.
umeongea vizuri ila nchi hii mambo ni magumu kuyabadiri, nchi haina hata vazi la taifa nchi gani hii
 
Back
Top Bottom