kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,839
- 20,285
Idara ya intelejensia nchini Ujerumani imesema kuwa, Korea Kaskazini ina jeshi la nne duniani na mpinzani wa nguvu wa Marekani.
Tovuti Ujerumani ya Astatysta na ambayo inajihusisha na ukusanyaji wa taarifa za kiintelejensia yenye makao yake mjini Hamburg, Ujerumani imeandika kuwa, kutokana na hatua ya Marekani ya kuelekeza meli zake za vita kuelekea katika pwani ya Korea Kaskazini, Pyongyang imeionya Washington kwamba, imejiandaa kwa ajili ya vita yoyote tarajiwa na Marekani.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Korea Kaskazini imeitahadharisha Marekani kwamba Washington inatakiwa ifikirie mara mbilimbili matokeo mabaya ya chokochoko zake hizo. Kuhusiana na hilo Pyongyang imetangaza kuwa, endapo meli hizo zitajaribu kufanya harakati yoyote ya kichokozi, basi Korea Kaskazini itawalenga kwa kuwashambulia marafiki wa Washington katika eneo hilo. Tovuti hiyo ya idara ya intelejensia ya Ujerumani imetathmini uwezo wa jeshi la Korea Kaskazini kwa kutegemea vyanzo vya ripoti za Kituo cha Kistratijia cha Kimataifa na kadhalika gazeti la The New York Times la nchini Marekani na kuandika kuwa, ikiwa mgogoro utaongezeka, Pyongyang inao askari wa kutosha kwa ajili ya operesheni za kukabiliana na waitifaki wa Marekani katika eneo la Peninsula ya Korea.
Kituo cha Kimataifa cha Utafiti wa Kistratijia chenye makao yake nchini Marekani kimeandika kuwa, Korea Kaskazini ina jeshi la nne duniani na kwamba uwezo wake katika kukabiliana na majeshi ya ardhini, haufai kupuuzwa. Inafaa kuashiria kuwa, Uchina ndio nchi yenye jeshi la pili duniani kwa kuwa na askari milioni mbili na laki mbili, huku India ikiwa na askari milioni moja na laki nne. Marekani ina jeshi la askari milioni moja na laki tatu, huku Korea Kaskazini ikiwa na jeshi lenye askari milioni moja na laki mbili.
Chanzo; parstoday.sw