Ujerumani kufanya uwekezaji mkubwa zaidi kuwahi kufanya Tanzania katika historia

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Mpango kabambe wa Industrialization ya nchi yetu unaendelea, hili ni bonge la uwekezaji unakuja Mkoani Lindi, 1 billion US Dollars!

Nasema vijana acheni blah blah nendeni Shule sasa tuchukuwe hizi kazi, fursa hiyo Imekuja nchini mwetu, Mungu atupe nini?
========

Shirika la petroli Tanzania kwa kushirikiana na muungano wa kampuni za Kijerumani zikiongozwa na kampuni ya Forrestaal wameingia ubia wa kujenga kiwanda kikubwa kwa ajili ya uzalishaji wa Mbolea. Uwekezaji huo utagharimu zaidi ya dola bilioni moja ya kimarekani.

Uwekezaji huo utakuwa ndio uwekezaji mkubwa zaidi kufanywa na ujerumani nchini Tanzania na wa kwanza kufanywa na Ujerumani kwenye sekta ya uzalishaji mbolea. Kiwanda kitaingia kwenye utendaji mwaka 2020 na kitazalisha tani milioni 1.3 kwa mwaka. Kiwanda kitajengwa kusini mwa Tanzania na kitatoa ajira 5,000.

Mkurugenzi wa TPDC, Dr James Mataragio amesema "Kwa maendeleo ya uchumi waTanzania hasa kwenye sekta ya kilimo, tunatarajia athari kubwa kutoka kwenye kiwanda. Kitaongeza thamani ya utengenezaji Tanzania. Sasa tunatazamia kuupeleka mradi kwenye hatua nyingine".

Kwa pamoja na washirika wa ndani, shirika la taifa la hifadhi ya jamii(NSSF) ambae ni muwekezaji mkubwa zaidi kwa mashirika ya umma na kampuni ya Mijingu ambae ni mzalishaji mkubwa na msambazaji wa mbolea kwa nchi za Afrika Mashariki, kati na kusini. Muungano huo sasa unafanya majadiliano kuhusu usambazaji wa gesi kwenye mradi.

Joint venture established to realise billion-dollar fertilizer-complex in Tanzania

Essen, 2015-10-28

TPDC, Ferrostaal, Haldor Topsoe and Fauji

The state-owned Tanzania Petroleum Development Corporation and a consortium led by the German company Ferrostaal Industrial Projects GmbH entered into a joint venture to realise a new world-scale fertilizer complex in Tanzania. The investment volume for the project will be more than one billion US dollar.

The petrochemical complex will be the largest German investment in Tanzania and the first fertilizer production in the country. It will be operational in 2020, producing 1.3 million tonnes of fertilizer per year. Located in the southern region of Tanzania it will provide 5,000 direct and indirect jobs.

Dr. James Mataragio, Managing Director of the Tanzania Petroleum Development Cooperation: “For the economic development of Tanzania, especially for the agricultural sector, we expect a huge effect from the plant. It will increase the value creation in Tanzania significantly. Now, we are looking forward to taking the project to the next level.” Together with its local partners Tanzania`s National Social Security Fund, the largest public investment fund in the country providing social security protection in Tanzania, and Minjingu Mines & Fertiliser Ltd, a major producer and distributer of fertilizer for East, Central and Southern Africa, the joint venture will now accelerate negotiations relating to the gas supply for the project.

“This agreement marks a major step forward to boost fertilizer production in Tanzania. The joint venture underscores our commitment to Tanzania to turn this important project into reality. Combining the competence of facilitating investments with the world`s leading technologies is our key to success”, states Dr. Klaus Lesker, Managing Director of Ferrostaal Industrial Projects GmbH, on behalf of the consortium of Ferrostaal with the Danish company Haldor Topsoe A/S and the Pakistani industrial enterprise Fauji Fertilizer Company Ltd.

Egon Kochanke, the German ambassador to Tanzania underlined: „The investment will be a milestone in the economic development of Tanzania. It will both strengthen Tanzania’s industrial base and its status as a new and attractive investment destination for Germany’s business champions.“

During a state visit of Germany`s Federal President Gauck in February the partners had already announced that the consortium led by Ferrostaal was the successful bidder for the development of the complex. This announcement followed a competitive tendering process.
About Ferrostaal Industrial Projects

Ferrostaal Industrial Projects is an international project developer and EPC service provider for the realisation of industrial plants in the wind energy sector as well as other selected project opportunities. The company additionally untertakes the planning, delivery, installation and maintenance of lighting solutions for sport and logistics. Ferrostaal Industrial Projects is a member of the Ferrostaal Group, a global technology-independent, manufacturer-independent and supplier-independent industrial services provider. Some 2,700 employees combine decades of industrial expertise with financing competence on behalf of the customers. Ferrostaal has own companies in around 40 countries.

SOURCE: Ferrostaal Group
 
Ni habari njema, kila jambo lina hatua. Ikiwepo mikakati na mipango bora nchi yetu itaendelea na kupiga hatua kimaendeleo.
 
Blah blah hizo tumezizoea,hao TPDC kila siku huja na plan wasizozitekeleza.Tatizo huwa inapotakiwa serikali itoe ahadi yake %ya uwekezaji inakua hakuna pesa.Mfano kiwanda cha NDC dawa za kuua mbu kibaha
 
Lakin isijekuwa kama waliko kamatwa wachina 360. Maana tulipewa hope lakin yanayoendelea huko ata sielew. Kama hiliswala litaendela kama kwa mheshimiwa macement. Itakuwa hakuna manufaa kwa watanzania. Uwekezaji wowote unatakiwa kuleta tija na manufaa kwa watanzania na sio tu kuishia kutumia natural resourse zetu na kunufaisha mataifa mengine akati sis tukibakia kuwa wanunuz tu wa bidhaa zilizozalishwa nchini kwetu
 
Blah blah hizo tumezizoea,hao TPDC kila siku huja na plan wasizozitekeleza.Tatizo huwa inapotakiwa serikali itoe ahadi yake %ya uwekezaji inakua hakuna pesa.Mfano kiwanda cha NDC dawa za kuua mbu kibaha

Kabla haujaandika kitu soma habari na uielewe, hiyo ni website ya kampuni ya ferostaal na siyo TPDC na hii ni kampuni ya Kimataifa hivyo mpaka waweke hilo kwenye front page yao ujue kitu kimesha take off!

Na isitoshe fedha kubwa inatoka Ujerumani, balozi wa Ujerumani TZ ameongea mpaka kamtaka Raisi wake hivyo hawezi kusema yote hayo kama ni blah blah tu!

Ferrostaal Industrial Projects
 
Akina Minjingu na wenzao wanatosha kwa hiki kilimo chetu cha mkono.

Ulishawahi kusikia neno Export? Sehemu kubwa ya mbolea itakuwa for export ili kuongeza pato la Taifa, Kiwanda kikubwa namna hii hakijengwi kwa ajili ya mbolea ya kutumika TZ TU, HAPANA!
 
Hii habari imeandikwa na mtu aliyelewa
Inafanya maneno ya msingi kwenye habari yaonekane kama udaku.

Huwezi kusema itakuwa kampuni ya kwanza Tanzania kuzalisha mbolea na wakati huo huo unataja Minjingu kama mzalishaji na msambazaji wa mbolea Afrika ya Mashariki na kati. Huu ni ulevi

Ila ni sawa tu kwasababu CCM ni walevi na naona imelenga zaidi uchaguzi wa 2020.

Hivi CCM, ule mradi wa mabasi yaendayo kasi uliosemekana kukamilika kipindi cha kampeni uko wapi?
Ilisemekana Gesi ya Mtwara ingeondoa kukatika kwa umeme pindi uzalishaji utakapoanza. Hivi hili likoje? Mbona bado unakatika?

Hangaikeni na vitu mlivyokwisha ahidi kwanza, acheni kuendelea kutoa ahadi, kampeni zimeisha. Fanyeni kazi ofisini na muache kuangaika na vyombo vya habari na maigizo ya kushona nguo.

Tanzania inahitaji rais zaidi kuliko fundi cherehani.
 
Yaani mtu aende shule leo kwa ajili ya kuja kuchukua kazi, kirahisi namna hiyo. Yaani hiyo kazi itakuwa inamsubiri yeye tu, acha unazi wa kipuuzi, unavosema vijana wanazungusha mikono na kumwabudu fisadi unalenga nini? Hata hiyo shule waende wapi? Mbona unayachukulia mambo kiwepesi namna hiyo, unadhani shule watu wanakwenda kwa miguu, shule ni kichwa. Kuwa mwangalifu wakati mwingine.
 
Nchi ambayo haina dira, hakuna tunalolifanya tumalize ndipo tuanze lingine. Tunashika shika tu kila sehemu. Yahani tunafanya shifting cultivation
 
Old wine in new bottle!! Alikuja Obama hapa juzi juzi tu....ukafunguliwa mradi wa several US dollars pale ubungo na tukaahidiwa mgao wa umeme utakuwa historia na tutauza umeme hadi kwa nchi jirani, yako wapi leo??

Tunaahidiwa uwekezaji wa viwanda katka nchi ambayo mwananchi anayetumia umeme chini ya megawatt moja kwa miaka kadhaa hawezi kupata umeme wa uhakika, vip kuhusi hivyo viwanda??! Mbona hizi ni habari za kuchekesha!

Acha muwa mtu wa kufurahia matukio, wenye akili huwa wanafurahia matokeo. Hatuwezi kuwa nchi ya viwanda mpaka pale tutapoweza kuzarisha nishati ya kutosha ya kuendeshea mitambo!! Huu ni ukweli ambao kila mwenye akili hawezi kuupinga.

Natumaini mradi huo huo hautokuwa danganya toto kama ule wa pale ubungo.
 
Hii habari imeandikwa na mtu aliyelewa
Inafanya maneno ya msingi kwenye habari yaonekane kama udaku.

Huwezi kusema itakuwa kampuni ya kwanza Tanzania kuzalisha mbolea na wakati huo huo unataja Minjingu kama mzalishaji na msambazaji wa mbolea Afrika ya Mashariki na kati. Huu ni ulevi

Ila ni sawa tu kwasababu CCM ni walevi na naona imelenga zaidi uchaguzi wa 2020.

Hivi CCM, ule mradi wa mabasi yaendayo kasi uliosemekana kukamilika kipindi cha kampeni uko wapi?
Ilisemekana Gesi ya Mtwara ingeondoa kukatika kwa umeme pindi uzalishaji utakapoanza. Hivi hili likoje? Mbona bado unakatika?

Hangaikeni na vitu mlivyokwisha ahidi kwanza, acheni kuendelea kutoa ahadi, kampeni zimeisha. Fanyeni kazi ofisini na muache kuangaika na vyombo vya habari na maigizo ya kushona nguo.

Tanzania inahitaji rais zaidi kuliko fundi cherehani.
Bora ata umeona hilo. Mie huwa najione huruma na hii Tanzania yangu. Kilakitu tunafanya kama tumekurupushwa. Mwekezaji anakuja hapa 95%+ job natural resources zote anachukua afu 5% ndo tunaachiwa afu tunachekelea tu. Hatupingi kuwa watalipa kodi lakini wawekezaji wengi wanaokuja Tanzania ni makanjanja.
 
Na ndiyo maana unatakiwa uache blah blah na uende Shule kama umeshazeeka basi peleka mtoto au ndugu, bila ya Elimu hakuna kazi kwani hata Muwekezaji pia anataka kuajiri MTZ ili asilipe gharama kubwa ya permit zaidi ya dola 2000 za kimarekani lkn analazimka kufanya hivyo!
Alafu kumbuka huyo mwekezaji ndo anayechagua nani wa kumwajiri. So akiamua ataleta watu wake na kuwaita ma expart. Kwasabababu nchii hii hakuna mtu mwenye ubavu wa kumuhoji mwekezaji. Atafanya anachojisikia na utaishia kulia lia tu na wanao kuwa hakuna kazi
 
Hii habari imeandikwa na mtu aliyelewa
Inafanya maneno ya msingi kwenye habari yaonekane kama udaku.

Huwezi kusema itakuwa kampuni ya kwanza Tanzania kuzalisha mbolea na wakati huo huo unataja Minjingu kama mzalishaji na msambazaji wa mbolea Afrika ya Mashariki na kati. Huu ni ulevi

Ila ni sawa tu kwasababu CCM ni walevi na naona imelenga zaidi uchaguzi wa 2020.

Hivi CCM, ule mradi wa mabasi yaendayo kasi uliosemekana kukamilika kipindi cha kampeni uko wapi?
Ilisemekana Gesi ya Mtwara ingeondoa kukatika kwa umeme pindi uzalishaji utakapoanza. Hivi hili likoje? Mbona bado unakatika?

Hangaikeni na vitu mlivyokwisha ahidi kwanza, acheni kuendelea kutoa ahadi, kampeni zimeisha. Fanyeni kazi ofisini na muache kuangaika na vyombo vya habari na maigizo ya kushona nguo.

Tanzania inahitaji rais zaidi kuliko fundi cherehani.

Duh! hata kusoma nako ni kazi jamani sasa mtasaidiwaje? Kwenye hiyo habari hakuna mahali ambapo pameandikwa kwamba hii itakuwa kampuni ya kwanza kuzalisha Mbolea bali imesema nanukuu ,,This agreement marks a major step forward to boost fertilizer production in Tanzania" au kikwetu makubaliano haya yataongeza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa mbolea Tanzania!
 
Back
Top Bottom