figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,485
Kasi ndogo ya ujenzi wa stendi kuu ya Songea inawatia wasiwasi wafanyabiashara waliohamishwa kwa muda kupisha ujenzi huo wakidai kwamba nyumba zao zipo hatarini kuuzwa na taasisi za fedha kutokana na mikopo waliyokopa kwa dhamana ya vibanda vya stendi
Channel ten imetembelea mradi huo na kukuta mafundi wakiendelea na kazi ambapo mhandisi msimamizi wa mradi huo Christopher Mpenda amesema mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi Januari 2016 mradi huo unatarajiwa kukamilika.
Mradi huo wa Stendi unagharimu shillingi milioni 500 fedha ya mkopo kutoka benki ya dunia.