PreGE2025 Ujenzi wa daraja la Magufuli (Kigongo-Busisi) lenye thamani ya bilioni 610, umefikia asilimia 97. Magari kuanza kupita Aprili 2025

PreGE2025 Ujenzi wa daraja la Magufuli (Kigongo-Busisi) lenye thamani ya bilioni 610, umefikia asilimia 97. Magari kuanza kupita Aprili 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
726
Reaction score
953

WhatsApp Image 2025-03-22 at 18.50.56_cb5065a6.jpg

WhatsApp Image 2025-03-22 at 18.50.49_3ac0e50b.jpg
Tarehe 22 Machi 2025, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) ilitembelea mradi wa ujenzi wa daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi) lililopo Mkoa wa Mwanza. Daraja hili, linalounganisha mikoa ya Kanda ya Ziwa na nchi jirani, lina urefu wa takriban kilometa 3.2 na linatarajiwa kubadili maisha ya wananchi.

Akizungumza mara baada ya kutembelea na kukagua daraja hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya PIC, Mheshimiwa Augustine Vuma, alisema kuwa mradi hilo lina thamani ya bilioni 610 na umefikia asilimia 97.

Vuma alieleza kuwa daraja hili litasaidia kupunguza muda wa kusafiri kwa kutumia vivuko kutoka masaa mawili hadi matatu hadi dakika tatu tu kwa gari.
WhatsApp Image 2025-03-22 at 18.50.50_c9872404.jpg
"Daraja hili litakuwa kivutio cha utalii na kitasaidia kukuza uchumi wa kanda ya Ziwa. Ni daraja la sita kwa urefu barani Afrika," alisema Vuma, akipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa juhudi za kufanikisha mradi huu.

Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Ambrose Pascal, alithibitisha kuwa daraja limefika hatua za mwisho na kuwa katikati ya mwezi Aprili 2025, magari yataanza kupita.

Amesema kuwa kazi inayofanyika sasa ni kumalizia kufunga taa, guard rail (uzio wa usalama), na kuweka alama za barabarani.

Aidha Kamati ya PIC imewataka wananchi kulinda miundombinu hii muhimu na kuwa walinzi wa mali za umma, ili kuhakikisha matumizi bora ya daraja hili.

Vuma amewataka Watanzania kuzingatia umuhimu wa kulinda miundombinu ya serikali kwa manufaa ya vizazi vijavyo.



=============================​

DARAJA LA J.P MAGUFULI KIGONGO BUSISI (KM 3 ), KUANZA KUTUMIKA APRIL 30

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Dkt. Charles Msonde amesema daraja la J.P Magufuli (Kigongo Busisi)KM 3 litaanza kutumika rasmi Aprili 30 mwaka huu.

Hata hivyo, amesema ifikapo Aprili 10, 2025 magari yataanza kupita upande mmoja kwenye daraja hilo ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 97.

Daraja hilo limejengwa kwa lengo la kuunganisha Barabara Kuu ya Usagara - Sengerema Geita KM90 ambayo ni sehemu ya barabara iliyopo kwenye Ushoroba wa Ziwa Victoria inayoanzia Sirari mpakani mwa Tanzania na Kenya hadi Mutukula mpakani mwa Tanzania na Uganda.
WhatsApp Image 2025-03-22 at 18.50.51_df93f04d.jpg
Kwa sasa sehemu ya barabara hiyo eneo la Kigongo Busisi inaunganishwa kwa kutumia vivuko vikubwa vitatu vya MV Mwanza, MV Misungwi na MV Sengerema.

"Kutokana na idadi kubwa ya magari yanayopita kwa siku, abiria na magari huweza kutumia muda wa takriban saa mbilii kuvuka kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine hivyo kukamilika kwake kutachochea maendeleo kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza" amesisitiza Dkt. Msonde.

Amesema baada ya daraja hilo kukamilika, muda wa kuvuka utapungua kufikia wastani wa dakika tatu (3) hadi nne (4) badala ya saa mbili ilivyo sasa.

Akizungumza leo Machi 22, 2025 wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma(PIC) ilipokagua ujenzi wa daraja hilo, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Msonde amesema Aprili 10, mwaka huu magari yataruhusiwa kuanza kupita kwenye upande mmoja wa daraja ambao utakuwa umekamilika kwa asilimia 100.

Daraja hilo lenye urefu wa kilomita 3 na upana wa meta 28.45 lina njia mbili za magari zenye upana wa mita 7 kila upande.

Dkt. Msonde amesema daraja hilo ambalo ujenzi wake umegharimu zaidi Shilingi ya bilioni 610 uimefikia asilimia 97.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, Augustine Vuma Holle ameipongeza Wizara ya ujenzi na Wakala wa Barabara (TANROADS) kwa kazi waliyoifanya kwenye daraja hilo, huku Kamati hiyo ikibainisha ni miongoni mwa miradi bora iliyoridhisha katika ukaguzi wa kamati hiyo.

"Hizi asilimia tatu zilizosalia mzikamilishe kwa wakati ili ifikapo Aprili 30, wananchi waanze kulitumia daraja hili na kuondokana na adha ya kuvuka kwa muda mrefu," amesema Vuma.

Mwenyekiti huyo wa (PIC), ameshukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na kueleza aliukuta mradi huo ukiwa umefikia asilimia 25 kutoka kwa mtangulizi wake, hayati John Pombe Magufuli na sasa umefikia asilimia 97.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI
 
Back
Top Bottom