Ujenzi bora wa chama CCM unategemea wana CCM wenyewe. Tujenge chama chetu kwa ufanisi na usasa

Ankoli

Member
Dec 17, 2017
48
24
Awali ya yote nitumie fursa hii kumshukuru Mungu muumba wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo, lakini pia namshukuru kwa kuijaalia nchi yetu kuwa na amani na utulivu ambao umefanya taifa letu kuwa na sifa kubwa dunia, lakini pia kwa kukijaalia chama chetu kuwa chama pekee chenye uwezo wa kutatua kero na shida za watanzania lakini pia kuwa tumaini la watanzania katika maisha yao.

Baada ya kutanguliza kusema hayo, nitumie fursa hii pia kutoa pongezi za dhati kwa Mhe John Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na pia kwa wajumbe wote wa Halmashauri kuu ya Taifa NEC, kwa sasa tunaweza kusema kuwa CCM imefanya usajili mpya wa timu ya ushindi kwa miaka 100 ijayo, hatuna mashaka na timu hiyo hata kidogo.

Kama wanachama wa Chama cha Mapinduzi tunajukumu kubwa na zito la kuhakikisha tuna waunga mkono viongozi wetu wapya na kutoa ushirikiano wetu wa dhati kwa ustawi na uimara wa Chama chetu.
Katika hotuba yake Mhe. Jakaya Kikwete katika mkutano mkuu wa Chama juzi alisema, moja ya changmoto kubwa ambayo kwa sasa chama kinapitia ni kuwa na wanachama wavivu wa kutoa ada za uanachama. Hivyo basi yatupaswa tutambue ya kuwa maendeleo ya Chama yanaletwa na sisi wenyewe, lakini pia ili cha kiweze kuganya shughuli zake bila kigugumizi lazima kiwe na msingi imara wa fedha.

Nakosa neno zuri la kusema kwa kumpongeza Mhe Magufuli kwa hatua nzuri na muhimu aliyo ichuku ya kuteua tume kwa nia ya kufanya tathmini ya miradi yote ya chama, hatua hii ni nzuri kwani itakisaidi chama kujua ni kiasi gani chama kinapata kwa mwaka kupitia miradi yake lakini pia kufanya uiano wa mapato hayo na miradi husika.

USHAURI WANGU KWA WANACHAMA.

1. Kutoa ushirikiano kwa tume hii pindi itakapo hitajika kupata taarifa husika juu ya miradi hiyo.

2. Kutoa mapendekezo yao kama wanachama ya namna bora ambayo miradi hiyo inaweza kutumika ikiwa kama sehemu ya kuongeza mapato ndani ya chama kupitia vyanzo vyake iwapo miradi hiyo inatumika chini ya matumizi bora.

3. Kutoa ushauri wao wa kubuni miradi mbadala ya kusaidia ukuaji wa mapato ya chama.

4. Mbali na mapendekezo hayo lakini pia Chama kuangalia namna gani kinaweza kwenda na usasa katika kubuni njia bora ya ukusanyaji wa mapato kwa njia ya ki elektroniki ili kupunguza mianya ya upotevu wa mapato, kuanzia ulipaji wa ada za wanachama hadi mapato ya miradi.

Nirudie kuwa omba ndugu zangu wapendwa wangu na wana ccm wenzangu, sisi ndiyo walinzi na wajenzi wa Chama chetu. Hakuna sababu ya kutofautiana na kuweka makundi kwani sote tunaishi katika nyumba moja. Jukumu letu kubwa la msingi ni kuhakikisha CCM inaendelea kuwa madarakani na kuisaidia serikali katika kutimiza majukumu yake.
Mwisho nirudie tena kumpongeza Mhe Magufuli Rais wetu mpendwa kwa kuamua kuubeba mzigo mzito wa kulitumikia taifa letu na chama chetu kwa maslahi ya taifa letu, na kwa watenfaji wote wa chama na serikali kwa kazi nzuri wanayo ifanya.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WANA JF.
 
Mpaka uote mkia siyo leo

Hapana ni dhamira njema na moyo wa uzalendo wa taifa langu tu mkuu.
Mimi ni mwanachama ambaye napenda chama changu sina nia ya kugombea wadhifa wowote katika chama, ila napenda kuwa sehemu ya chachu ya mabadiliko na mafanikio makubwa ndani ya chama changu kwa maslahi ya Taifa letu.
Mchango na nguvu zangu uweze kuongeza ladha nzuri na utamu wa CCM

CCM OYEEEEEEE
 
CCM ni ya wajinga, wazee na maskini, sijui mkuu upo kundi gani?
 
Hapana ni dhamira njema na moyo wa uzalendo wa taifa langu tu mkuu.
Mimi ni mwanachama ambaye napenda chama changu sina nia ya kugombea wadhifa wowote katika chama, ila napenda kuwa sehemu ya chachu ya mabadiliko na mafanikio makubwa ndani ya chama changu kwa maslahi ya Taifa letu.
Mchango na nguvu zangu uweze kuongeza ladha nzuri na utamu wa CCM

CCM OYEEEEEEE

Mtaacha lini kutumia mapanga dhidi ya wapinzani wenu kisiasa? Je jeshi la polisi litaendelea kuwasaidia mpaka lini katika uga wa siasa?
 
Mtaacha lini kutumia mapanga dhidi ya wapinzani wenu kisiasa? Je jeshi la polisi litaendelea kuwasaidia mpaka lini katika uga wa siasa?

Kwa dhati ya moyo wangu na uchungu mkubwa sana nasikitika kuona kama vijana wa tanzania wana amini hayo unayo sema.
Nasikitika kwa sababu hakuna ushahidi wa kuthibitisha hayo usemayo, lakini nasikitika pia kuona kuwa unaumizwa na jinsi ya jeshi la polisi linavyo tekeleza kazi yake vema na kwa weledi kwa ajili ya ulinzi wa raia na mali zao.
Nilitegemea ungetoa sifa na pongezi nyingi kwa polisi wetu kwa kutuliza ghasia ambazo zinaweza kuvuruga amani ya nchi yetu.
 
Sitegemei wewe kuweza kuona unyama wanaofanyiwa wapinzani kwasababu unasoma magazeti ya uhuru na mzalendo na kutazama TBC1 peke yake. Jitahidi ubaki hukohuko kwenye giza. Jeshi la polisi ndio linaratibu kupigwa na kuumizwa kwa wapinzani kwa sababu ccm haina uwezo wa kujenga hoja za ushawishi bali mabavu. Sasa ili kuwasaidia ccm hatutoshiriki uchaguzi unaondeshwa kinyama na kikatili, ni bora mshindane na jeshi la polisi mtaamua nani atatangazwa mshindi, ila kiukweli hamna uwezo wa kufanya siasa za ushindani.
 
Suala si siasa za ushindani bali ni siasa zenye uwezo na nia njema ya kulikomboa taifa na watanzania, ni siasa yenye kujali misingi ya utu , usawa, haki na umoja wa kitaifa, siasa ambazo ni mhimili madhuburi wa ujenzi wa uchumi wa nchi yetu na usalama wa taifa letu.
Si siasa za kubagua na kugawa watanzania kama mafungu ya nyanya sokoni, siasa za kuleta uadui na kuvuruga umoja wa taifa letu.
Ni CCM pekee ndicho chama kina siasa za kistaarabu, zisizo na matusi wala kejeli na ndiyo maana pamekuwapo na mlipuko wa upinzani kuhamia CCM kutokana na sera zake nzuri, uongizi imara na mipango mizuri kwa taifa letu.
 
Sitarajia mshabiki wa simba aseme simba ni dhaifu? Huo uchambuzi wako na sifa ulizomwagia ccm ingekuwa iko madarakani kwa ridhaa ya wananchi hapo sawa, ila sio kwa kutumia tume dhaifu na jeshi la polisi huku rushwa ikiwa kete muhimu. Hakuna chama chenye siasa za matusi, bali kuna siasa za kusema ukweli na vijembe vya kisiasa ni sehemu ya mchezo wa siasa. Ila kwakuwa ccm ni chama cha kizee, kimebaki kutegemea propaganda ili kubaki madarakani.

Hata Kanu ya Kenya, UNIP ya zambia vilikuwa vinaongopea wananchi kwamba vyenyewe ndio vyenye kuweza kuongoza nchi hizo. Ila vimeondoka madarakani na mambo yanasonga tena mazuri kuliko kwetu ccm inapong'ang'ania madaraka. Hao wapinzani wanaohamia ccm ni baada ya kuhongwa kwani ccm inaweza kuchota hela hazina bila ruhusa na kuzitumia ipendavyo.
 
Unajua kirefu cha UKAWA?
Ujinga Kawaida kwa Wapinzani

Sasa ukisema CCM Chama cha wajinga umesikia sisi tuna jiita ukawa

Kama huna ukionacho kizuri kati ya shehena ya mazuri yanayo fanya na CCM chini ya uongozi imara Mhe Magufuli, nina mashaka makubwa utakuwa huna mapenzi hata na familia yako.
 
Kama huna ukionacho kizuri kati ya shehena ya mazuri yanayo fanya na CCM chini ya uongozi imara Mhe Magufuli, nina mashaka makubwa utakuwa huna mapenzi hata na familia yako.

Halafu wewe unaonekana lazima ni mzee maana naona unajiquote mwenyewe na propaganda zilizopitwa na wakati. Kalee wajukuu siasa za hoja huziwezi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom