Ujauzito wa wiki ishirini na mbili

Step by step

JF-Expert Member
Apr 28, 2014
1,160
1,283
Habarini wana jf.
Mke wangu ana ujauzito wa wiki ya 22 na ndio mimba yake ya kwanza hivyo sina uzoefu sana wala mwenyewe hana uzoefu.
1. Kuna mama ametuambia kuwa kipindi hiki cha ujauzito wife asinywe maji ya baridi yatasababisha mtoto azaliwe akiwa na matatizo ya kifua je pana ukweli hapa?
2. Mtoto anacheza lakini mara chache sana. Anaweza cheza asubuhi tu mpaka asubuhi tena je ni sahihi kwa mimba ya umri huu?
Clinic nahudhuria ila tu najua humu pana wazoefu hebu mwenye kila wazo jema la kushirikishana kipindi hiki ntalipokea kwa upendo
 
5 to 6 Months (20 to 24 Weeks):
clip41.jpg

Kufikia wiki 20 "koklea" ambacho ni kiungo cha kusikia, umefikia kiwango cha mtu mzima ndani ya sehemu ilikamilika mwa sehemu ya ndani ya masikio. Kuanzia sasa na kuendelea, kijusu ataanza kuhisi Sauti ya vipimo mbali mbali.

3555.jpg

Nywele zaanza kumea kichwani.

Sehemu muundo rusu wote wa ngozi Umekamilika, Ukiwemo mizizi ya nywele na tezi.

clip42.jpg

Kufikia wiki 21 hadi 22 tangu kutunga mimba, mapavu hupata uwezo kidogo ya kufuta hewa. Umri huu huitwa umri ya "kujikimu" kwa sababu uwezo wa kuishi nje ya nyumba ya mtoto huwezekana kwa baadhi ya vijusu. Uwezo wa utaalamu wa utibabu huleta uwezekano ya kudumishwa kwa maisha ya watoto walio zaliwa kabla ya wakati.

Angalia:BIOLOJIA YA UKUAJI WA MTOTO TUMBONI

 
Aisee hiyo ya maji sidhani kama inaukweli. Wengine tumekunywa maji ya baridi hadi dakika ya mwisho hayakuketa madhara.....

Kikubwa ale vizuri balanced diet asiache vidonge vya wajawazito na mazoezi muhimu
 
Aisee hiyo ya maji sidhani kama inaukweli. Wengine tumekunywa maji ya baridi hadi dakika ya mwisho hayakuketa madhara.....

Kikubwa ale vizuri balanced diet asiache vidonge vya wajawazito na mazoezi muhimu
shikrani ndugu ntazingatia
 
Wiki ya 18-25 ndio mtoto uanza kucheza, kama ameannza na 22 basi Heri itakapofika 25 ataruka viduku kabsa....
Maji ya baridi huwa salama tu maana watoto wengine viburi mpk umpige Maji ya baridi ndio ushtuka... So mama akitaka amuamshe anapiga Maji baridi dogo anaruka
 
poa so hakuna muingiliano wowote wa baridi ya yale maji na mtoto alieko tumboni?manake wife anapenda ya baridiiiiiiii haswa ndo anatulia
 
Back
Top Bottom