Kuna kila sababu ya mtanzania kusema "HAPANA" na kuamua kuchukua hatua madhubuti za kupambana ujangili (poaching) ambao ni tatizo kubwa ktk nchi yetu na ndani ya bara la Afrika.
Tanzania imejaliwa vitu vingi vya thamani kama wanyama pori wakiwamo Tembo na Faru ambao leo wapo ktk hatari ya kutoweka dunia kutokana uwindaji mbaya na uliopitiliza wanaofanyiwa usiku na mchana,kwenye giza na kwenye mwanga.
Majangili au wawindaji hao haramu ni wale tunaowaweka ktk kundi la majangili wakubwa na wa hatari zaidi(LARGE SCALE POACHING) Ambao wao hawana huruma kwa viumbe hao.
Tembo na faru wapo ktk hatari ya kupotea ktk uso wa dunia na wakti huo huo ni ktk wale wanyama wakubwa (BIG FIVE)huku wakiwa na sifa za pekee ikiwemo ya kutoa vipuri (TROPHY) ambazo ndizo vivutio vikubwa kwa majangili hao.
Ifike siku sasa,watanzania tuchukue hatua madhubuti za kupambana na majangili hao na kuwatokomeza kabla ya wao hawajatokomeza wanyama wetu.
Pato kubwa la nchi litazidi kupotea kila siku iwapo ujangili utazidi kufumbiwa macho.