Ujambazi wa Tanzania ni baraka za dhati za watawala wa Tanzania.

Bernard bakari

JF-Expert Member
Mar 30, 2016
407
781
Swala la Ujambazi katika Nchi ya Tanzania ni jambo linalotikisa nchi mara kwa mara. Kwa wakati tofauti tumekuwa tukishuhudia matukio ya kijambazi sehemu mbalimbali nchini Tanzania, Majambazi hao wamekuwa wakitumia silaha kali kama mabomu na bunduki.

Tumeshuhudia vituo vya polisi vikivamiwa na silaha kuchukuliwa rejea tukio la stakishari, mabenki yakivamiwa na pesa kuchukuliwa tena mabenki yanavamiwa na silaha za moto kama bunduki

Baada ya Tukio la ijumaa la mkuu wa mkoa kuchukua Askari 6 wakiwa na bunduki najiuliza walipata wapi bunduki hizo, je Askari huwa anakaa nyumbani na Bunduki, je wale ni walinzi wake? Kama mkuu wa mkoa anakuwa na nguvu ya kuamuru askari kwenda kuvamia kituo cha habari cha clouds atashindwaje kuchukua Askari wenye silaha za moto na kuwaamuru wakavamie benk za NMB, CRDB, NBC nk.

Naanza kuvuta hisia kama waziri wa mambo ya ndani, waziri wa ulinzi, mkuu wa majeshi, mkuu wa polisi, RPC wote tanzania, Wakuu wa mikoa wote Tanzania, Wakuu wa wilaya wote Tanzani wanatuaminisha vipi kuwa hawatumii Askari katika namna hii ambayo kama si CCTV kunasa uovu mpk leo tusingetambua uozo unaofanywa na viongozi wetu juu ya kutumia vyombo vya dola kufanya uhalifu.

Naamini na nitaendelea kuamini kuwa Ujambazi unaoendelea nchini Tanzania si bure ni baraka za dhati zinazotolewa na Viongozi wetu kwa hali hii watanzania tushirikiane wananchi wenyewe kwenye kupambana na Ujambazi kutegemea askari na viongozi ni ndoto za abunuhasi. MUNGU IBARIKI TTANZANIA
 
Back
Top Bottom