Daniel Mjema
Member
- Jul 23, 2007
- 77
- 84
Ndugu zangu,
Jana usiku kulitokea ujambazi huko Tanga ambako watu wanne waliuawa. Juzi saa 8:00 usiku wa kuamkia jana majambazi wakiwa na silaha walipanga mawe eneo la Mgagao wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro na kuwapora madereva na abiria wa malory. Ukitizama mfululizo wa matukio ya ujambazi nchini utakubaliana na mimi mambo muhimu yafuatayo:-
1. Bado usalama wa Taifa hawawajibiki ipasavyo maeneo yao ili kukusanya taarifa za uhalifu na wahalifu wanaotishia usalama wa nchi. Zamani walikuwa hawafahamiki, walijichanganya na wananchi kukusanya taarifa. Leo baadhi ya maofisa usalama wa taifa(sio wote) wanaona hadi ufahari kujitambulisha au kutambuliwa na jamii
2. Jeshi la Polisi linapaswa kusukwa upya ili liendane na mabadiliko ya sayansi na tekinolojia ambapo wahalifu hasa majambazi, wanatumia akili nyingi kupanga matukio. Jeshi la polisi lifuatilie nyendo za polisi wake waliofukuzwa baada ya kutiwa hatiani na mahakama zao za kijeshi. Wachunguzwe wanafanya shughuli gani maana hadi miaka ya 80,polisi akifukuzwa alikuwa akirejeshwa hadi kijijini kwao na kumkabidhi kwa uongozi wa kijiji. Leo hii tuko nao uraiani lakini hawajulikani wanafanya kazi gani kujiingizia kipato. Wako ambao ni wema lkn wapo ambao ulikosekana tu ushahidi wa kuwatia hatiani katika mahakama za kiraia japo kwenye mahakama ya kijeshi walitiwa hatiani. Kitengo cha Intelijensia cha polisi kiimarishwe ili kukusanya taarifa sahihi za wahalifu na uhalifu wasijikite kutafuta tu taarifa za kiintelijensia pale kunapokuwa na mivutano ya kisiasa kuhusu maandamano na mikutano ya vyama vya siasa hasa hasa upinzani. Jeshi la polisi litambuliwe linakabiliwa na changamoto kubwa ya uhalifu wa kimakundi hasa uhalifu unaojikita kwenye mwavuli wa dini.
3. Mhimili wa mahakama nao utimize wajibu wao katika kutenda haki. Wasiwe wanatafuta visingizio vya dosari za kiufundi ili tu kumwachia mtu aliyepatikana na hatia ya wizi wa kutumia silaha. Jaji au Majaji wa mahakama za rufaa watazame ushahidi wa jumla kama una uzito kiasi gani badala ya baadhi yao kutafuta vidosari vidogo vidogo vya utaratibu wa uendeshaji wa kesi lower courts ili tu kuhalalisha kuwaachia watuhumiwa sugu wa ujambazi. Wajue wahalifu hawa iko siku watabisha hodi kwenye nyumba zao hata kama sio kwa Jaji au Hakimu aliyemwachia lkn hata kwa coleague. Uzoefu unathibitisha kuwa wengi waliofungwa miaka 30 kwa ujambazi wa kutumia silaha wanapoachiwa hurudi kujihusisha na uhalifu tena kama mwanzo alifungwa kwa kutumia kisu anaporudi hupanda daraja na kutumia bunduki au bastola.
4. Kuna haja ya kukiingiza cheo cha Balozi wa Nyumba kumi kumi kuwa chro rasmi cha kiserikali. Mtakumbuka baada ya sheria ya mfumo wa vyama vingi hawa walibakia kuwa viongozi wa CCM ambao huchaguliwa na mkutano mkuu wa Shina la CCM. Tutafute njia bora ya kupatikana kwao, kama ni kutumia utaratibu ule ule wa kumchagua mwenyekiti wa mtaa au wa kitongoji ni sawa ili awe na uhalali wa kuwa kiongozi wa kiserikali wa kusimamia nyumba hizi kumi. Ili mgeni yeyote katika hizo nyumba kumi lazima aandikishwe kwa balozi wa eneo husika ametokea wapi, amekuja kwa shughuli gani, mwenyeji wake ni nani na liwe sharti la lazima kuja na uthibitisho wa barua kutoka katika nyumba zile kumi anapotokea. Hii itasaidia kuwatambua watu wanaoletwa na kuhifadhiwa katika mitaa yetu halafu usiku wanakwenda kufanya uhalifu
5. Sisi kama raia hatujatimiza wajibu wetu kikamilifu kwa kufichua mipango ya uhalifu na wahalifu. Wala tusijitetee. Wahalifu hawa tunaishi nao na ni ndugu, jamaa na marafiki zetu. Pilikapilika za uhalifu zinaweza kuonekana katika mitaa yetu. Tuzitilie mashaka pilikapilika hizi hasa zinapohusisha wageni mitaani kwetu. Tusiguswe kufichua uhalifu tu pale tunapoguswa moja kwa moja kwa ndugu au jamaa kuuawa au kuporwa na hata kujeruhiwa. Tusisubiri kwa sababu uhai huwezi kuununua dukani.
Watanzania tukiamua, tunaweza kuupunguza uhalifu
Siku njema