Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,221
- 2,425
Kuna wale watu wanawekaga password kwenye simu zao halafu wanasahau kabisa wanajikuta wanataka ku format simu zao ๐ bila kupenda ??
Relax kuanzia Leo kama umesahau password kwenye simu Yako una haja ya kuformati simu !! Kuna kitu kinaitwa Google smart lock ๐
Google smart lock inakusaidia wewe kufungua simu yako kwa urahisi Sana ikiwa una tabia ya kusahau password kufungua simu.
Ikiwa uko nyumbani utaki Kila mara ukitaka kupokea simu au kutumia simu kuweka password ndo utumie au umetumiwa ujumbe huwezi kusoma mpaka utoe lock wakati huko nyumbani.
Google smart lock wamekuwekea njia Rahisi ya kuweza ku set simu Yako ikiwa Uko maeneo to Fulani basi password ijiondoe automatically isiwepo Ila ukiwa pia ukiwa mahali Fulani basi simu Yako huwezi kutumia mpaka huweze kutoa lock ya password au pattern Yako.
Mifumo hii imegawanyika katika sehemu kuu tatu ๐
๐บ On body detection
Mfumo huu unafanya kazi ikiwa unataka kutoa simu kwenye begi lako basi kupitia mwili wako kwa kuchezesha mkono, kunyoosha juu google smart lock haitakuuliza password yenyewe automatically tu inajitoa.
Ila mfumo huu ๐ jamani jihadhari Sana maana mtu yeyote anaweza kufungua
๐บ Trusted device
Kupitia njia hii utaweza kuchagua kifaa ambacho unakiamini Kama simu , tablet , laptop nk. Ivyo ikiwa simu Yako umewasha tu Bluetooth na imeunganisha na kifaa kingine , automatically password inatoka.
๐บ Trusted place / location
Kupitia njia hii utakua una set location ambayo unaiamini, unaweza kuchagua maeneo ya nyumbani au kazini kwako. Ivyo ukiwa hayo maeneo una haja ya kuingiza password unatumia tu Kawaida simu Yako.
Jinsi ya kuseti google smart lock ni rahisi Fanya Hivi
1. Ingia setting kwenye simu 2. Security 3. Chagua smart lock kama ujaiona endelea advanced settings >> smart lock>> utachagua Sasa unataka Nini kati ya izo setting
Je umeshawahi kutumia google smart lock au ndo tunakujuza Leo tuachie maoni Yako ?