Uhusiano wenye "taswira ya kizee"

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
40,187
Reaction score
62,256
Mahusiano yanatakiwa yawe na furaha na matumaini. Sasa unakuta watu wako kwenye mahusiano yasiyokuwa na furaha au matumaini ya kufikia hatua fulani, unakuta kunakuwa na upenzi au uchumba sugu uliodumu zaidi ya miaka 4 hakuna ndoa wala dalili ya kufikia ndoa.

Pia, kuna ndoa zingine migongano mara kwa mara, kama walilazimishwa kuoana. Unakuta huyu anachepuka Kaskazini mwingine anachepuka Kusini. Ukiona hizo dalili, jua huo ni uhusiano wenye taswira ya kizee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…