UHUSIANO/URAFIKI BORA.

ndammu

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2017
Posts
5,442
Reaction score
6,379
Usivunje uhusiano na mtu sababu tu umegundua kuwa sio rafiki. Kwenye maisha hatuhitaji marafiki tu bali tunahitaji watu wote.

Kila mtu atakufaa kwa namna tofauti,hata wale wasio marafiki kuna kipindi watakufaa.

Sio kila mtu atakufaa kwenye biashara au kipindi unatafuta kazi na sio kila mtu atakufaa kipindi unajiandaa na harusi yako au kipindi unatafuta mtu wa kukukopesha.

Pia, sio kila mtu atakufaa kipindi unaumwa au kipindi umefiwa.

Jambo moja tunalokosea ni kudhani kuwa yupo mtu atakayetufaa kwa kila kitu. Na kwa namna hiyo tumepoteza watu wengi ambao wangekuwa na manufaa kwetu,Anaekufaa kwa kila kitu ni Mungu pekee[color]. Binadamu wote watakufaa tu kwa msimu.

Kinachotakiwa ni kutambua kila mtu anaekuzunguka anakufaa kwa nini, na kumtumia kwa hicho ambacho anakufaa. Usivunje uhusiano/urafiki wa miaka mitano sababu tu hakuja msibani ulipofiwa. Ndani ya miaka mitano hakukufaa kwa jambo jengine lolote lile?

Chumvi haitakufaa kwa chai asubuhi, ila itakufaa kwa mboga mchana.

Kila mtu atakufaa katika jambo tofauti na katika nyakati tofauti.

Mahusiano bora huongozwa na akili na sio hisia.

Majukumu mema nyote.

Tenha um bom dia por tudo.
 
Na usikumbatie kumbatie watu ambao kwako ni hasara, bora kuwapotezea
 
[emoji122][emoji122][emoji122]

"Tusiache mbachao kwa msala upitao"hayo ya waswahili..,.binadamu tunategemeana sana sana hakuna aliye bora dhidi ya mwenzake,.muhimu ni kujua nafasi yako na yao hao(wakuzungukao) ili kuepuka baadhi ya mambo yaso muhimu kwenye maisha yako kwa wakati huo.

Tupendane,tuheshimiane,tuvumiliane na mengine mazuri-zuri maana hatujui kesho yetu.

Zaidi sana MUNGU wetu mwema atukumbushe fadhili zake.
 
Umenena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…