trem
JF-Expert Member
- Sep 19, 2014
- 340
- 201
Watu mbalimbali watasikia ujumbe was aina moja na kwa wakati mmoja, lakini tafsiri zao zitakuwa tofauti
Kwanini inatokea hivyo?
1.kila mtu (hata ndani ya jamii/kabila moja) anao uhuru wa kutafsiri tukio, ujumbe, kitu, au tatizo fulani kwa namna anavyoelewa yeye na kutegemea jinsi alivyolelewa kuelewa uhalisia wa mambo.
2.mtu hutafsiri matukio, ujumbe, vitu au matatizo kutegemea uzoefu aliokwisha pata maishani na uhusiano wake binafsi na tukio lenyewe.
3.Aidha, tafsiri ya mtu binafsi hutegemea mambo mengine kama yafuatayo:-
a. Mila na desturi(utamaduni) zake
b. Uzoefu wake maishani
c. Kudhania kwake (presuppositions) kunakotokana na mazoea
d. Mkutadha aliyomo
e. Matukio ambayo ameyapitia kabla ya kile anachosikia au kukiona sasa
f. Uhusiano halisi wa mtu mwenyewe na tendo au kitu kinachotokea sasa
g. Kutegemea hali ya hisia za mtu mwenyewe
h. Kutegemea umri wa mtu anayehusika
4.mtu hutafsiri ujumbe au mambo kwa namna mbalimbali .maana ya jambo au neno haimo katika maneno tu. bali pia katika maswali , kwa mfano, kwann? wapi? lini? na pia kwa kutegemea ni kwa mtu wa aina gani ujumbe unatolewa .
a. Msemaji ana uhusiano gani na msikilizaji
b. Ni nini kinachomchochea msemaji kusema anayosema.
Kwa ujumla kila kitu msikilizaji aonacho, awazacho, na kusikia huwa ni sehemu ya ujumbe unaotolewa
Karibu kwa maoni na mawazo zaidi