AZUSA STREET
JF-Expert Member
- Oct 31, 2013
- 2,007
- 1,894
1. Kaimu Jaji mkuu upo hapa, tunaomba mahakama mtusaidie.
2. Majaji wanaoharibu kesi zetu tutawashugulikia.
3. Wakili wa kujitegemea anayetetea washitakiwa, na yeye aunganishwe kwenye mashitaka...kwanini anatetea waovu?
3. Mawakili wa serikali, majaji na mahakimu wanaoharibu kesi zetu tutawashughulikia.
4. Wakili aliyetetea watuhumiwa anakamatwa na polisi.
5. wakili anatoka mahakamani halafu anakamatwa na polisi kutokana na kumtetea mtuhumiwa.
2. Majaji wanaoharibu kesi zetu tutawashugulikia.
3. Wakili wa kujitegemea anayetetea washitakiwa, na yeye aunganishwe kwenye mashitaka...kwanini anatetea waovu?
3. Mawakili wa serikali, majaji na mahakimu wanaoharibu kesi zetu tutawashughulikia.
4. Wakili aliyetetea watuhumiwa anakamatwa na polisi.
5. wakili anatoka mahakamani halafu anakamatwa na polisi kutokana na kumtetea mtuhumiwa.
kwa wanasheria au mtu yeyote mwenye uelewa na sheria, tutakuwa sahihi tukisema Tanzania hakuna uhuru wa mahakama, au kuna uhuru wa mahakama?
Hivi nini maana ya Haki inatakiwa kuonekana imetendeka sio tu kuwa imetendeka. hata watu wa pembeni wakiangalia utaratibu uliotumika, wanatakiwa kuiona haki ikiwa imetendeka.
Halfu,
1. Nayeunda kesi hadi kushinda ni nani, kati ya polisi/mpelelezi, prosecutor/wakili wa serikali na majaji/mahakimu?
2. Polisi akiunda kesi yake vizuri, imepelelezwa vizuri, prosecutor atakuwa na sababu gani kushindwa kesi?
3. Prosecutor akipresent kesi yake kwa hakimu/jaji vizuri kama ilivyopelelezwa vizuri na mpelelezi, Jaji/hakimu atakuwa na sababu gani kuipiga chini?
4. tumlaumu nani sasa, aliyeshindwa kupeleleza, aliyeshindwa kupresent, au aliyepokea ushahidi dhaifu usiopelelezwa vizuri akaona hakuna jinsi ila kuipiga chini?
kwanini tunawalaumu mahakimu/majaji waziwazi bila kuangalia nyuma ya pazia kilichotokea? tunajuaje kama pengine ushahidi unaopelekwa mahakamani huwa ni ushahidi uliopelelezwa vibaya na wapelelezi wasio wazuri, na kuwa presented na prosecutor dhaifu asiyejua sheria na anayepambana na upande unaojua sheria?
hivi hii nchi tupo kwenye kiota? watu hawatakiwi kudai haki kwasababu hakimu nii mtu fulani tu? uhuru wa mahakama upo au haupo? kwanini mawakili wa kujitegemea, majaji na mahakimu, mawakili wa serikali wanadharauliwa wakati wao hawaendi field kukusanya ushahidi au wakati wao kisheria(advocates) wanatakiwa kuwatetea watu kwa kuisaidia mahakama kufikia haki kwa ushahidi uliokusanywa na sio kwa ushahidi wa kutungwa? hata kama ni kweli mtu amefanya, kama ushahidi uliopelekwa ni dhaifu, hakimu/jaji gani atamtia hatiani mshitakiwa, na precedent hiyo hata vizazi vijavyo vitasema huyo jamaa akili yake ilikuwaje kumtia hatiani mtu ambaye ushahidi haujakua presented kuprove kosa?
katiba inasemaje? kila mtu anatakiwa kuhesabiwa haki hadi chombo maalumu kitamke kuwa ana hatia, na ni kwa procedure zilizowekwa na sheria, sio procedure za kisiasa? Mungu atusaidie.