Sasa angeshiriki ingesaidia nini labda?
Chaguzi zetu washindi wanajulikana kabla ya uchaguzi, watawala wanaandaa uchaguzi kwakua ni matakwa ya katiba, wanaandaa namna ya kushinda iwe kwa nguvu au kwa wizi na uchaguzi ukiisha wanafanya sherehe za kujipongeza
Hii ni sawa na kujitekenya na kucheka mwenyewe.
Yule wa UG anakomaa kubadilisha katiba, yule wa Rwanda nae anahakikisha katiba inamruhusu kuongoza mwanzo mwisho, na mpinzani anayejitokeza anamtia shida mpaka wengine waogope kujitokeza, kule kwa Mugabe anajitahidi anaongoza mpaka anaingia kabulini, Kule kwa Nkurunziza ni vichekesho tupu.
Bara la Africa ni aibu tupu unaweza kuhisi sisi wote ni wehu