Things like this is why cord is gaining two points and going 5 back...sasa how can he learn from JPM ???? HE DOESNT HAVE THAY POWER .....EVEN IF AM CORRUPT UHURU CANNOT FIRE ME BY WORD OF MOUTH BUT BY COURT OR PARLIAMENT!!
Hata ukishikwa red handed? Hizi katiba hizi zina faida na madhara mengi sana sumtyms.
That's why mmefeli. (Miserably)Mimi nakuhakikishia Magu akipewa urais Kenya atatamani kuutema siku hiyo hiyo ya kwanza. Kuwaongoza Wakenya kwa kutumia mikwara, ubabe na vitisho ni vigumu sana, inabidi ufuate utawala wa sheria na mifumo iliyopo ya kikatiba. Huko tulitoka zamani zile za Moi eti kwamba rais angeweza kumfuta na kumwajiri yeyote na popote na kwa wakati/muda wowote anaotaka au kufikiria au kuwaza.
Rais Uhuru alijaribu na ameishia kuheshimu sheria baada ya kutafsiriwa Kenya ya leo sio ile ya zama za babake.
Halafu vipi pamoja na mikwara ya kwenu mumefikia wapi ufisadi Bongo kama Lugumi, IPTL, escrow na mengineyo.
Wewe kubali kuwa Uhuru hana ujasiri wa kushughulikia ufisadi, acha kujificha nyuma ya kivuli cha katiba. Watu kama Anne Waiguru walikuwa chini yake lakini hakuwa na ujasiri wa kuwafuta kazi kutokana na yeye mwenyewe Uhuru kutokuwa msafi. Watu wote wanaofutwa kazi na Magufuli wapo chini ya uteuzi wake. Usitake kutudanganya hapa kuwa katiba ya Kenya inaruhusu ufisadi.Mimi nakuhakikishia Magu akipewa urais Kenya atatamani kuutema siku hiyo hiyo ya kwanza. Kuwaongoza Wakenya kwa kutumia mikwara, ubabe na vitisho ni vigumu sana, inabidi ufuate utawala wa sheria na mifumo iliyopo ya kikatiba. Huko tulitoka zamani zile za Moi eti kwamba rais angeweza kumfuta na kumwajiri yeyote na popote na kwa wakati/muda wowote anaotaka au kufikiria au kuwaza.
Rais Uhuru alijaribu na ameishia kuheshimu sheria baada ya kutafsiriwa Kenya ya leo sio ile ya zama za babake.
Halafu vipi pamoja na mikwara ya kwenu mumefikia wapi ufisadi Bongo kama Lugumi, IPTL, escrow na mengineyo.
Mimi nakuhakikishia Magu akipewa urais Kenya atatamani kuutema siku hiyo hiyo ya kwanza. Kuwaongoza Wakenya kwa kutumia mikwara, ubabe na vitisho ni vigumu sana, inabidi ufuate utawala wa sheria na mifumo iliyopo ya kikatiba. Huko tulitoka zamani zile za Moi eti kwamba rais angeweza kumfuta na kumwajiri yeyote na popote na kwa wakati/muda wowote anaotaka au kufikiria au kuwaza.
Rais Uhuru alijaribu na ameishia kuheshimu sheria baada ya kutafsiriwa Kenya ya leo sio ile ya zama za babake.
Halafu vipi pamoja na mikwara ya kwenu mumefikia wapi ufisadi Bongo kama Lugumi, IPTL, escrow na mengineyo.
Hehehe!! Mnavyotiririka... hadi raha, naona mumeguswa penyewe. Ndio hapo, utawala wa sheria na mifumo ya kikatiba ndio dawa, lakini hayo ya kufoka na mikwara utaishia kuwababaisha watu wa chini lakini kule juu wanakuangalialia kwenye hatua kumi na nane zao.
Kenya hatujafika, lakini hatua zilizopo ni chanya, tunatoka na tunaenda, gurudumu linazunguka tu... mafisadi wanaburuzwa mahakamani hadi kero. Sio kazi rahisi maana yalikua yamekita mizizi, watu walizoea kuiba na kulindwa na mifumo ya uongozi, leo hii hata rais hana uwezo wa kukulinda. Mawaziri wake hata wale wa karibu naye walinyofolewa, alijaribu kukwama nao, lakini mfumo uliopo haukumpa fursa au nafasi ikabidi aachie tu.
Tutafika tu, na tunakwenda tena kwa kasi. Leo hii jaji mkuu hateuliwi na rais, inabidi Wakenya wenye uwezo wajitokeze na kujieleleza uwezo wao na sifa zao tena mbele ya runinga ya taifa. Hiyo ndio taswira hata kwenye nyadhifa zingine nyeti....taasisi na mifumo ndio ngao yetu, sio mihemko ya mtu mmoja ambaye kila siku inabidi watu wakae makini wakimsubiri hawajui ataibuka na lipi leo.
Gikuyu, Embu, and Meru Association (GEMA). Waembu na Wameru (wa Kenya) ni jamii za Kikuyu kwa kiasi kikubwa.Kwani GEMA ndo nini?
Manyang'au bana!!! Pamoja na uwazi wa katiba yenu rushwa imepaa kwa kasi ya ajabu!! Tulikwisha acha ligi na nyinyi maana hakuna jipya. TZ tuna style yetu kujirekebisha, kwanini mnataka kujilinganisha? Umesema gurudumu linazunguka; well good for you!! Nasisi linazunguka kwa style yetu- whay comparison?
Subiri tu baada y amiaka kumi tutaongea vizuuuri...na mtatuelewa.
"The sleeping giant awakens"
Hatuwezi kuruhusu wanasiasa kutumia majanga kama njia ya kutafuta kiki. Upuuzi kama Wa Uhuru na Raila hatuwezi kuachia kwenye jamii yetu iliyostaarabika.Inabidi tujilinganishe ili kukumbuka tulikotoka na kushukuru. Yaani kwenu hata upinzani hawana ruhusa ya kutoa misaada kwa waliokutwa na majanga. Najaribu kupata picha leo hii eti akina Raila ambao ni viongozi wetu wa upinzani itokee wanakwenda kutoa misaada sehemu halafu wazuiliwe na mapolisi kama mlivyomfanya Mbatia.
Kama nilivyosema, bado hatujafika tunakokwenda, lakini tukiangalia nyuma yetu na kuona majirani waliko, inabidi tukubali kwamba hatua tumezipiga nyingi. Uganda kule kiongozi wa upinzani anaishi jela, ila bora wao huthubutu kupinga wasilolitaka, lakini Bongo ndio usingizi kabisaaaa.