Wambugani
JF-Expert Member
- Dec 8, 2007
- 1,757
- 277
Ingawa misitu ni chanzo cha maji na huvutia mvua, Kijiji cha Masabeda ambacho kipo juu ya ukuta wa Bonde la Ufa maarufu duniani, ipo katika Wilaya ya Karatu inapuuza kanuni hiyo ya utunzaji wa mazingira na hivyo kuruhusu wananchi kukata miti kiholela kiasi cha kusababisha uharibifu wa mazingira.
Pamoja na kasi ya Rais wa Awamu ya Tano, Mh. Dk. John Magufuli, hata viongozi wa Wilaya wameonekana kutokujali uharibifu huo wa mazingira ambayo ni adha kubwa kwa Taifa. Pichani ni moja ya lundo la miti, ambayo ni uoto wa asili iliyokatwa katika Kijiji cha Masabeda tayari kwa kuchomwa kwa ajili mkaa jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya uhifadhi wa misitu.
Kila siku asubuhi wananchi wa Vijiji vya Masabeda na Endalah huonekana mjini Karatu wakiwa wamebeba kuni na makaa kutoka msitu huo unaotegemewa kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira muhimu kwa ajili ya Ziwa Manyara.