Andre02150
JF-Expert Member
- Feb 2, 2010
- 332
- 129
Naomba msaada kwa wenye kuelewa sheria za kazi zinasemaje pale mtumishi (mwanamke) anapopewa uhamisho na mwajiri wake pasipo kuzingatia ndoa yake.
Hivi karibuni taasisi nyingi za umma ikiwemo TRA zimekuwa zikihamisha wafanyakazi na hivyo kupelekea kutenganisha familia. Kuna wanawake wenye ndoa na watoto wadogo wamejikuta wanahamishwa pasipo kuzingatia ndoa zao. Swali ninalouliza je sheria ya ajira inasemaje juu ya married couple? Nani anatakiwa amfuate mwenzie inapotokea uhamisho? Je mwajiri ana nafasi gani katika ustawi wa familia na jamii kwa ujumla? Hivi mwajiri anapohamisha watumishi na hatimae kutenganisha wanandoa haoni kama ameshindwa kumtendea haki mtumishi wake?
Nafikiri ni wakati muafaka kwa Serikali, taasisi za kijamii kuona umuhimu wa kuliangalia hili suala kwa macho ya ukaribu kwa ajili ya kujenga familia bora.