mputamaseko
JF-Expert Member
- Apr 1, 2013
- 1,401
- 949
kumekuwa na kucheleweshwa kwa stahiki mbalimbali za watumishi wa umma tokea awamu hii hiingie madarakani kutokana na sababu mbalimbali , moja wapo wa haki zinazocheleweshwa ni hii ya uhamisho kwa watumishi wa umma kutoka kituo kimoja kwenda kituo kingine. Naomba kupitia uzi huu wadau mbalimbali wanao guswa tuutumie kuikumbusha serikali yetu kuwa kuna familia nyingi za watumishi ambao wanaonana mara mbili au tatu tu kwa mwaka, hii inasababisha msongo wa mawazo na inaweza kusababisha migogoro mikubwa sana ndani ya familia na jamii zetu. Naomba ifikie hatua viongozi wetu watambue kuwa wamechaguliwa kutumikia watu, muda mwingine wajivike uhusika wa watu wanao waongoza! Naomba serikali iruhusu uhamisho ili wafanyakazi waungane na familia zao popote pale walipo nchini.
Karibuni sana wadau tuchangie kistaarabu na kwa lugha ambayo sio ya kukwaza kikundi ama mtu yeyote. Wasalaam