Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,525
- 22,465
Nikiwa nje ya Tanzania niliwahi kubadilisha pasi yangu ya kusafiria mwaka 2006.
Wakati ule pasi ile ya kusafiria ilichukua miezi karibu saba kabla ya kuipata nikiwa nipo nje ya Tanzania,na hasa kwa kutumia ubalozi kutuma maombi kwa niaba yako nchini Tanzania.
Pia nakumbuka wakati ule watanzania waliokuwa nje walikuwa wakilipishwa ada ya kusafirisha pasi hizo lakini pesa (paundi 100) hiyo ikiishia mikononi mwa wachache.
Lakini hivi karibuni zaidi ya wiki mbili zilizopita nilifanya maombi ya kubadilisha pasi yangu baada ya kuisha muda wake.
Lakini kwa kwa sababu za urasimu wa nmna ya kuipata pasi hiyo pia nikawa na wazo jingine kwamba kwa kuwa kwa sasa kuna serikali mpya na Idara ya UHAMIAJI imebadilishwa, si vibaya nikijaribu kutuma maombi yangu nchini Tanzania.
Nilichokifanya ni kumtumia bahasha iliyokuwa na maombi ndani yake ndugu yangu alieko Tanzania ambae nae aliipata wiki iliyopita na kuipeleka moja kwa moja UHAMIAJI siku ya Alhamisi.
Vijana wa Idara hii wakapokea maombi yangu na kuahidi kuyashughulikia ndani ya wiki moja, lakini haikupita wiki pasi ikawa tayari na Ijumaa iliyopita pasi ikatumwa na wao wenyewe UHAMIAJI kuja moja kwa moja kwangu kupitia DHL.
Napenda kushukuru sana kwa kuona ufanisi ulioonyeshwa na Idara hii ambayo kwa miaka mingi imekuwa na matatizo ya urasimu na rushwaambapo kuna wakti ilibidi uwaone vishoka ili mtu uwezi kupata pasi ya kusafiria.
Ni utaratibu mzuri sana ambao UHAMIAJI wameanzisha ambapo maombi yakifika Dar-es-Salaam yanapokelewa na baada ya kushughulikiwa UHAMIAJI wanaweza kukutumia pasi yako kupitia DHL badala ya kupelekwa Ubalozi wa nchi unayoishi.
Ni imani niliyo nayo kwamba hii sera ya "hapa kazi tu" ifikie maeneo yote yaliyokuwa na kero kama ARDHI HOUSE, TANESCO, DAWASCO.