Uhalisia wa mshahara wa mwalimu baada ya makato mapya ya 15% ya Bodi ya Mikopo ya elimu ya juu

Bornventure

JF-Expert Member
Jan 29, 2017
529
523
Uhalisia wa mshahara wa mwalimu baada ya makato mapya ya 15% ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu.

Baadhi ya makato katika mshahara wa mwalimu ni kama inavyoonekana kwenye mabano;-

Mfuko wa hifadhi ya jamii (35,800 sawa na asilimia 5%)

Bima ya afya (21,480 sawa na asilimia 3% )

CWT (14,320 sawa na asilimia 2%)

Bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu -HESLB (107,400 sawa na asilimia 15 %)

Income tax (86,580 sawa na asilimia 12%).

Jumla ya Makato tu ni tsh 265,580/=.

Mwalimu anayelipwa mshahara wa tsh 716,000/= anabakiwa na tsh.450,420/= kwa ajili ya kuchangia michango iliyowekwa kwa shuruti na kugharamia maisha yake.

Kila mmoja apige hesabu kutokana na mshahara wake, bila kusahau kuweka makato ya mikopo kutoka kwenye taasisi mbalimbali.

Baada ya hapo kinachobaki kipeleke kwenye matumizi yako binafsi:-

1. Maendeleo
2. Chakula
3. Kodi ya pango
4. Umeme
5. Maji
6. Usafiri
7. Mawasiliano
8. Shughuli za kijamii
9. Tegemezi
10.Michango ya mwenge, maabara, madawati nk.
11. Matibabu yasiyo kwenye bima.
12. Mavazi

Pamoja na makato hayo, hakuna;-

1. Posho ya usumbufu wala muda wa ziada.

2. Posho ya usafiri kwa wanaokaa mbali na kituo cha kazi kutokana na mazingira.

3. Posho ya makazi, nk.

Inamhitaji mwalimu kuwa mzalendo wa kupita kiasi, ama kuzuga, ama nidhamu ya woga katika kutekeleza majukumu yao.

Serikali, chama cha walimu CWT na vyama vya wafanyakazi kwa ujumla embu oneni aibu juu ya hili.

Elimu haichezewi.
 
Mfuko wa hifadhi ya jamii (35,800 sawa na asilimia 5%)
MAKATO ya LAZIMA

Bima ya afya (21,480 sawa na asilimia 3% )
MAKATO ya LAZIMA

CWT (14,320 sawa na asilimia 2%)
MAKATO ya LAZIMA

Bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu -HESLB (107,400 sawa na asilimia 15 %)
Hayo ni MAKATO ya KUJITAKIA

Income tax (86,580 sawa na asilimia 12%).
Haya ndio MAKATO YA LAZIMA.

- Sasa kama wewe ULIKOPA Ukala BATA, Lipa MADENI, Usifikiri kila mtu anadaiwa kama wewe na anapata makato kama yako.
 
>Mwalimu anaruhusiwa kulima bustani au mazao ya msimu.

>Mwalimu anao mda wa kufuga kuku nguruwe ama mifugo mingine.

>Mwalimu anayo fursa ya kufungua tuition center baada ya mda wa kazi.

>Mwalimu anao mda wa kufungua Bar(kuanzia sa kumi jioni hadi sa sita usiku)

>Mwalimu asipo kua mainder(kutafuta cheo kwa kuchapa watoto bila sababu eti uogopwe ili upewe cheo)kuna mda mwingi sana anao wa kufanya ujasiriamali.

TATIZO LENU WALIMU:
Mnafata palipo na wepesi wa maisha kama umeme, maji na barabara bila kujua mda ulio nao ni wakutafuta maisha sio wa kupumzika!

Nakubaliana na walimu kua mazingira ya kazi ni mabaya kwao lakini haingii akikini mwalimu kijana unahama kituo cha kazi jombe vijijini ambapo ungeweza kulima na kufuga kwa miaka kadhaa na ungeweza kuwa mbali kimaendeleo ILA utakuta mtu kutwa na mibahasha anataka ahamie Dar bila ya sababu ya msingi inayo zidi fursa alio iacha pori!

Acha mfwe tu na njaa maana ndio mnacho kiweza japo mlinifundisha kusoma na kuandika ila kuna mda siwa elewi KABISA!
 
hqdefault.jpg
 
>Mwalimu anaruhusiwa kulima bustani au mazao ya msimu.

>Mwalimu anao mda wa kufuga kuku nguruwe ama mifugo mingine.

>Mwalimu anayo fursa ya kufungua tuition center baada ya mda wa kazi.

>Mwalimu anao mda wa kufungua Bar(kuanzia sa kumi jioni hadi sa sita usiku)

>Mwalimu asipo kua mainder(kutafuta cheo kwa kuchapa watoto bila sababu eti uogopwe ili upewe cheo)kuna mda mwingi sana anao wa kufanya ujasiriamali.

TATIZO LENU WALIMU:
Mnafata palipo na wepesi wa maisha kama umeme, maji na barabara bila kujua mda ulio nao ni wakutafuta maisha sio wa kupumzika!

Nakubaliana na walimu kua mazingira ya kazi ni mabaya kwao lakini haingii akikini mwalimu kijana unahama kituo cha kazi jombe vijijini ambapo ungeweza kulima na kufuga kwa miaka kadhaa na ungeweza kuwa mbali kimaendeleo ILA utakuta mtu kutwa na mibahasha anataka ahamie Dar bila ya sababu ya msingi inayo zidi fursa alio iacha pori!

Acha mfwe tu na njaa maana ndio mnacho kiweza !
Chungu kumeza
 
Back
Top Bottom