Uhalali wa migomo ya CHADEMA

Uhalali wa migomo ya CHADEMA

RABIN GHYOOT

Member
Joined
Sep 17, 2014
Posts
10
Reaction score
2
Ukisoma "Tanzania Daima" la jumatatu, tarehe 15th September 2014 ukurasa wa mbele unaona kichwa cha habari "Migomo, maandamano bila ya kikomo nchi nzima", "Mbowe aonya sasa basi, amshukia Sitta."

Pia ukisoma "Tanzania Daima" la jumatano, tarehe 17th September 2014 ukurasa wa tano unaona kichwa cha habari "Maandamano yaiva" humo ndani kuna taarifa na nukuu "Taarifa kutoka Makao makuu ya Chadema na mikoani zinaeleza kuwa maandalizi ya maandamano ya amani na migomo isiyo na kikomo yenye lengo la kushinikiza kusitishwa kwa shughuli za Bunge Maalumu la Katiba inaendelea kukamilika."

Baada ya kusoma hizi taarifa naona CHADEMA wanachanganya vitu viwili tofauti "Migomo" na "Maandamano"

Ingekuwa haya magazeti hayamilikiwi na Mbowe na hawa waandishi hawakuajiriwa na Mbowe ningefikiri ni uzushi.

Kinachoshangaza katika mpango wa Mbowe ni "migomo". Kufanya au kuhamasisha migomo bila ya kuwashirikisha TUCTA ni uvunjifu wa sheria.

Ukiangalia sheria ya kazi na ajira unaona wanaoweza kugoma ni wafanyakazi kupitia vyama vyao, tena baada ya kupiga kura kwa mujibu wa katiba ya chama chao. Pale wengi wamepiga kura ya kuchagua kugome ndio mgomo unafanyika.

Section 80(1)(d) of Employment and Labour Relation Act 2004 inasema:

"employee may engage in lawful strike if the strike is called by trade union, a ballot has been conducted under the union's constitution and majority of those voted were in favour of the strike"

Kwahiyo kuitisha mgomo kwa namna yoyote nyingine ni kuvunja sheria.

Vilevile kuna makundi yanayotowa huduma muhimu yamekatazwa kugoma na sheria za nchi.

Kwa mfano makundi yanayotowa huduma za maji, umeme, afya, zima moto nakadhalika.

Kwahiyo Mbowe anavyo hamasisha kugoma bila ya kufafanua anavunja sheria za nchi.

Kwahiyo waislamu wanapohoji inawezekana vipi Mbowe anavunja sheria lakini anaachiwa huru, wakati Sheikh Ponda alipovunja sheria alitiwa ndani wana hoja ya msingi.

Je ni dhamana gani mtu anapewa ambayo masharti yake yanaruhusu mtu kutoka nje ya nchi? Basi hata Sheikh Ponda angepewa ili akimbie zake mpaka mambo yakipowa.


Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inazungumzia Mkusanyiko kama haki ya msingi ambayo pia inawajibu wake (duty).
 
  • Thanks
Reactions: gsu
...

.....swaga magamba !!!

102_6487.jpg
 



Mtoa mada naona kama akili zako ndo kama za huyu mbunge! wa CCM! hembu nitajie chama cha wakulima/Biashara/wanabodaboda/madereva ambacho ni coutry wide na chenye usajili kama ilivyo CWT,TUGHE ,TALGU
 
Last edited by a moderator:
kwa bahati mbaya zaid uelewa wa mbowe ni mdogo sana yeye huamini mandamano na vurugu ndiyo zitakuza chama chake kumbe anajidanganya kabisa.
 



Mtoa mada naona kama akili zako ndo kama za huyu mbunge! wa CCM! hembu nitajie chama cha wakulima/Biashara/wanabodaboda/madereva ambacho ni coutry wide na chenye usajili kama ilivyo CWT,TUGHE ,TALGU


wewe unatakiwa kupewa dozi kubwa sana ndiyo upone vinginevyo unakwenda kuchanganyikiwa kabisa.
 
Last edited by a moderator:
hapa mbowe amepanga kukusanya watu wasiokuwa na ajira rasmi, watagoma kukaa bila kazi, hili ni lazima tuunge mkono, vijana lazima wagomee kukaa bila kazi ya kuwapa kipato, shida ajira ya mbowe ya kuandamana bila kikomo haina tija, maCCM hawawezi kusikiliza kilio cha mbowe na vijana hawa. Instead tuwape elimu, tuwaambie vijana ajira yao ipo kwenye ballot box, tuwaandae kuwatoa maCCM kwa njia ya kura, tuwaandae kulinda kura kama Iringa kwa Msigwa, hapo tutakuwa teyari kufia kura zetu.
 
Back
Top Bottom