Uhakiki wa kauli za serikali, iundwe tume huru

afsa

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
1,986
1,585
Kumekuwa na tuhuma nyingi kuelekea kwa SERIKALI ambazo mara zote hukanushwa na serikali kupitia kwa waziri mwenye dhamana.

Mara nyingi tuhuma zinapokanushwa huishia hapo.
Napendekeza iundwe tume huru itakayakuwa ikihakiki majibu ya tuhuma dhidi ya serikali ili tuweze kuwa na taarifa sahihi kwa kila tuhuma.

Mara kwa mara SERIKALI inapotuhumiwa hukanusha haraka sana.

Mfano wa tuhuma ni Rais kutofuata sheria, haraka mwanasheria wa serikali amekanusha, mfano wa pili tuhuma za wakuu wa wilaya na mikoa kutofuata sheria zimekanushwa, mfano wa tatu mifuko ya hifadhi ya jamii kuhisiwa kufilisika wenye dhamana wamekanusha, mifuko iko salama.

Iundwe tume huru itakayokuwa inafuatilia tuhuma na majibu kuihusu SERIKALI na tuhuma zinazoikabili ili kuepuka uongo wa pande zote mbili.
 
Hii serikali inatufanya watanzania Mazuzu.Hao wasomi tunaowategeme watutete sisi wanyonge wamekaa kumya.kazi kufuata mkhumbobo tu. Kwa kweli kauli nyingi za viongozi wa serikali ni za ajabu sana, hasa kiongozi mkuu. Eti viongozi wanao watetea wahalifu washitakiwe!!! .Huyu jamaa anajifanya yeye yuko juu yasheria!!!! Mimi sio mwanasheria lakini kwa upeo wami sioni kama kuna shiria inayomkataza mwanasheria kumtetea muhalifu.Mahakama pekee ndio yenye kumuona mtu mwenye hatia,na kama mahakama yenyewe ikifuata sheria sio kumtia mtu hatani kwa amri toka juu.
 
Hata aliyoongea juzi yatakanushwa hakusema au hakuwa anamaanisha hivyo.Ni Serikali ya Matamko yenye hisia za chuki na Ubaguzi
 
Back
Top Bottom