dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,500
- 3,481
Wananchi wa kijiji cha Sukuro kata ya Komoro katika wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wapo hatarini kukumbwa na magonjwa mbalimbali kutokana na kutumia maji ya bwawa yasiyo safi na salama sambamba na wanyama wafugwao na wa msituni wanaotoka katika hifadhi ya Tarangire.
Kutokana na hali hiyo,wameiomba Serikali kulipatia ufumbuzi tatizo la maji katika kijiji hicho chenye zaidi ya wakazi elfu sita ambao wao na mifugo huchangia maji ya kunywa bila kujali madhara wanayoweza kuyapata kutokana na kutokuwa na njia nyingine ya kupata maji zaidi ya maji ya bwawa hilo.
Kutokana na adha hiyo Taasisi isiyo ya kiserikali ya ECLAF Foundation ya Manyara kupitia kwa Mwenyekiti wake Peter Toima imesema iko mbioni kuanza ujenzi wa mtambo wa kuchuja maji ya bwawa hilo na kuyawekea dawa ili yawe safi na salama kwa ajili ya matumizi ya wananchi huku Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mahmud Kambona akieleza kuwa wilaya hiyo inatoa huduma ya maji kwa wananchi wake kwa asilimia 39 na kwamba jitihada zinafanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau ili kuongeza asilimia ya wananchi wanaopata maji safi na salama.
Chanzo: ITV