Escardo-bird
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 622
- 220
Niliuguwa nikiwa kidato cha tano, nikarudishwa nyumbani ili nisiambukize wengine shuleni, Nilipata homa kali sana ambayo sijawahi kuumwa tena, niliabukiza watoto wote walio kuwa wadogo kwangu hasa under 13yrs, huo ugonjwa siupendi na nauogopa, sipendi uikumbe familia yangu hasa nikikumbuka unavyoleta homa kali, hadi leo ninamakovu manne ya huu ugonjwa ili hali niliugua miaka 10 iliyopita.
Yaah nasikia nilazima upate hata ukiwa mkubwa lakini sipo sure kabisa kwa hilo vip wewe hujawahi pata nini
Yaah nasikia nilazima upate hata ukiwa mkubwa lakini sipo sure kabisa kwa hilo vip wewe hujawahi pata nini
Umenipata Mwaka 2012 Nipo Chuoni Nilikuwa Naona Hadi Aibu Kutoka Nje Njinsi Nilivyokuwa Natisha
Daah mkuu hadi leo bado vikovu bado unavyo, yaan huu ugonjwa unakereketa vile vipele vyenye maji vinawasha afu unaambiwa usivikune arrrrghhhh tukiwa wadogo bro aliugua akawa anasugua mgongo kwa ukuta ajikune vipele vya mgongo kwa pamoja yaan unatesa sana.
Kiukweli Huu Ugonjwa Unatisha Mbona Hatuoni Wazungu Wakiuguu Ina Maana Uko Afrika Tu
Makovu ya huu ugonjwa ni balaa, nawaza dengue ingekuwa inaambukiza kama tetekuwangu sijui tungekuwa wapi sasa, maana inaambukiza haraka sana
Mimi niliugua mwaka jana nilikua nina mtoto mchanga wa miezi miwili nilizipata chuo kuna dada alikua anaugua na tulikua kipindi cha mitihani akashindwa kuahirisha. Niliteseka saana maana zilinitoka mwili mzima hadi kwenye chuchu nilikua nasikitika kumnyonyesha mwanangu. Tulikua nyumba nzima na mwisho wa siku akaugua mwanangu nilimuwahisha hospital akapewa dawa ya kunywa na kupaka haxikutoka zaidi ya vipele vitatu tu nikamshukuru mungu. Ila niliteseka saaana usoni nilikua kma nimebandikwa tope. Ila nimebaki na alama chache sana.
niliungua mwaka 2008, ulipoanianza sikujua ndio ugonjwa wenyewe ila vipele vilikuwa vinaongezeka kila baada ya muda mfupi, nakumbuka nilitoka vipele hadi kwenye kichwa