Ugonjwa wa Alzheimer | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugonjwa wa Alzheimer

Discussion in 'JF Doctor' started by Kitia, Mar 30, 2009.

 1. Kitia

  Kitia JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2009
  Joined: Dec 2, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Napenda kuuliza kama kuna mtu yeyote anayefahamu jina la ugonjwa wa Alzheimer kwa kiswahili. Natanguliza shukrani.
   
 2. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,186
  Likes Received: 680
  Trophy Points: 280
  Mkuu, swali zuri sana hata mie ningependa kufahamu ila nina wasiwasi kama huu ugonjwa una jina la kiswahili!
   
 3. Kitia

  Kitia JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2009
  Joined: Dec 2, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Usemalo ni kweli. Huu ni ugonjwa ambao umeanza kuwa diagnosed siku hizi za karibuni. Mara nyingi huwapata watu kuanzia miaka 65. Itokeapo hivyo watu huchukulia kuwa ni dalili za uzee, kusahau n.k. Ugonjwa ukiendelea mgonjwa huanza kuchanganyikiwa, kusahau matukio, watu n.k. Natumaini mpaka sasa wengi tunafikiria kuwa mzee amechanganyikiwa, au amekuwa kichaa, ila ni athari za huu ugonjwa. Ingawa ugonjwa huo haujapata tiba bado, kuna dawa za kupunguza makali na kuusimamisha mahali ulipofikia usiendelee. Ugonjwa usipodhibitiwa, husababisha kifo. Mpaka sasa familia yangu imeathirika na wazee wawili, na nafahamu familia zingine tatu ambazo wazee wao wamekumbwa na ugonjwa huo.

  Kuna haja ya kuifahamisha jamii kuhusu ugonjwa huo na athari zake, namna ya kuudhibiti na namna ya kutoa malezi kwa wagonjwa. Vile vile kuna haja ya kuangalia jinsi sheria inavyoweza kumlinda mgonjwa maana imetokea mara nyingi mgonjwa kutapeliwa mali zake kutokana na hali hiyo ya kuchanganyikiwa.
   
 4. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2009
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kitia umesema"Mpaka sasa familia yangu imeathirika na wazee wawili, na nafahamu familia zingine tatu ambazo wazee wao wamekumbwa na ugonjwa huo."
  Kwa hiyo utakuwa una uzoefu mkubwa -unaweza kutusaidia jinsi ulivyowasaidia hao wazee wako na jinsi ulivyousimamisha usiendelee bila dawa kama ulivyosema?Asante.
   
 5. Kitia

  Kitia JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2009
  Joined: Dec 2, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwa bahati mbaya, mzee mmoja alipoanza kuugua, tulijua kuwa amechanganyikiwa kwa ajili ya uzee. Hali iliendelea hivyo hivyo na kwa bahati mbaya akafariki. Kwa sababu hapakuwa na diagnosis ya kutosha, wala autopsy, hatukuweza kujua kwa uhakika kuwa ni kitu gani kilichomuua. Ilikuwa ni rahisi zaidi kuona dalili hizo kwa mzee wetu wa pili. Tulimleta kututembelea huku ughaibuni, ndio tukagundua kuwa tabia yake imebadilika kabisa, anasahau sana, na mara nyingi matamshi yake hayaleti maana. Hapo ndipo tukampeleka hospitali, akafanyiwa medical check up, psychiatric analysis na pia kufanyiwa MRI scan ya ubongo. Vipimo vilionyesha kuwa tayari ameshambuliwa na huo ugonjwa wa alzheimer. Daktari alitueleza hakuna dawa za ku reverse effects za ugonjwa huo, ila kuna dawa amabazo zinaweza kufanya ugonjwa huo usiendelee zaidi. Kwa mfano, hataacha kusahau, lakini rate ya kusahau itabakia palepale, badala ya kuendelea. Mojawapo ya dawa hizo ni Vitamin E (IDO-E9) pamoja na Arisept, au Doneratio, dawa ambazo mpaka sasa anatumia. Hata hivyo, dawa hizo, hasa hizi mbili za mwisho hazipatikani Tanzania, na imebidi tuwe tunatuma kila mara. Hizo anatakiwa kunywa maisha.

  Care ya mgonjwa wa alzheimer ni ngumu sana kwa mgonjwa, na wewe unayetoa huduma. Kisaikolojia ita ku affect sana ukiona mzazi wako amebadilika amekuwa na hali hiyo. Mara nyingi atakuudhi kwa maneno yake, na inahitaji uvumilivu na upole katika kutoa huduma. Vilevile kuna haja ya kumpatia mgonjwa mental exercises ili aweza kutumia ubongo. Michezo kama karata, bao nk husaidia. Vile vile inabidi kumpa majukumu ya kufanya kutokana na uwezo wake.

  Kutokana na kwamba ugonjwa huu umeanza kuonekana kwetu, kuna haja ya kuelimisha umma kuhusu athari zake. Vilevile kuipa sekta ya afya uwezo wa ku diagnose na kutoa matibabu, ambayo inabidi kupata dawa hizo kwa bei nafuu. Kama nilivyosema awali, kuna haja ya kuangalia jinsi sheria itakavyowalinda watu waliathirika na ugonjwa huu.
   
 6. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Hivi ni wewe uliyeuliza jina la ugonjwa huu kwa kiswahili?nilikuwa najaribu kuangalia kamusi ya magonjwa ghafla nikaona maelezo yako yanaelekea kutoa jibu nikahisi labda ulikuwa unatoa kitendawili sasa naona unasubiri mji.
   
 7. Kitia

  Kitia JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2009
  Joined: Dec 2, 2006
  Messages: 410
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Asante mkuu. Sisubiri mji hata kidogo. Natafuta mchango wa jumuia kutaka kujua zaidi kuhusu ugonjwa huu katika jamii yetu. Naomba nisieleweke kivingine.
   
 8. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,186
  Likes Received: 680
  Trophy Points: 280
  Ni kweli ugonjwa wa Alzheimer unahusishwa sana na umri mkubwa kwa sababu hutokea zaidi kwa watu wazima/wazee. Kwa ufupi husababishwa na aina fulani ya protini (amyloid beta) ambayo huunganika pamoja na kusababisha seli za ubongo kutofanya kazi ipasavyo. Dalili zake ni kama ulizozitaja. Wataalamu wa afya (madaktari) wanaweza kutuelezea kwa undani zaidi. Kwa Tanzania inawezekana ukawa umeanza kuwa diagnosed au kufanyiwa utafiti katika siku za karibuni ila kwa nchi kama USA utafiti ulianza zamani. Alzhemier ni mojawapo kati ya magonjwa yanayo waathiri wamarekani kwa wingi.
   
 9. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  BONDIA,muhamed ali, si anao ugonjwa huu,au nimechanganya,yeye wanasema kaupata sababu ya kupigwa mangumi
   
 10. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,186
  Likes Received: 680
  Trophy Points: 280
  Ugonjwa wa Muhamad Ali unaitwa Parkinson, ni tofauti na Alzheimer japo nao pia unashambulia ubongo.
   
 11. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #11
  Mar 30, 2009
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Asante SANA Kitia-bora mtu ukala chako mapema kabla ya age hiyo. Maana umenikumbusha nilipokuwa age 7,kazi yangu ilikuwa ni kushughulika na babu yangu,ambaye kwa unavyozungumza naona kwa zaidi ya 75% alikuwa na ugonjwa huo,maana nilikuwa namwambia twende kula,yeye anazungumzia mambo ya benki au mke wake anamuuliza unanijua anasema ndio wewe si Mr.so and so,wao. looh uliponimaliza nguvu sasa ni hizo dawa kuwa hazipatikani uswahilini,yaaani hapo ndio watu kwa kuepuka kifo wanajivua uzalendo kwenda kuishi sehemu ambayo ikinifika hali hiyo angalau nipate kidonge.
   
Loading...