!
!
watu sahihi wa kusuluhisha huo ugomvi ni wewe mwenyewe na mke wako mkuu. Rudini na mtafakari upya kwamba ni yapi yalikuwa malengo na matarajio yenu na kama bado hayo matarajio yenu na malengo yapo hivyo. Angalieni pia matokeo, Mmefanikisha kipi na kuvurunda wapi. Mjaribu kupima kupitia hayo ili kujua kama, na matokeo huwa yanakuwa ya aina mbili tu hapa "ni ama mnaachana au mnaendelea", kama mnaachana haina shida, achaneni kwa amani tu kwani ni matokeo na mtakuwa na ya kujifunza, kama mtaendelea basi muendelee kwa namna ambayo mahusiano hayawi mzigo, yaani mbadilike msameheane mheshimiane. Msipotezeane muda, kama imeshindikana ni bora mkaachana kila mtu akatafuta ustaarabu wake.
Ni hayo tu
Ni wewe mwenyewe... sio nyie na mkeo wala mtu mwingine.
Narudia tena, mpatanishi sahihi ni wewe MWENYEWE (ALONE)...
Kama wewe ndiye uliyekosa, kubali kujishusha, uombe msamaha na ujitahidi usirudie tena
Kama (unaamini) ni mkeo aliyekosa, kubali kumsamehe bila masharti yeyote
Kama ni wote mmekoseana, kubali kuyabeba yote mwenyewe, then omba msamaha, mwambie wife ...naomba yaishe mke wangu...
Ukishirikisha "watu" sana sana unaweka kovu lisiloisha kwenye ndoa yako...
Hivi mkuu unajua "kisa" cha Franswaa kuimba huu wimbo?
Mkuu, mimi nadhani tena sio yeye na mke wake... Ila yeye mwenyewe. Mkewe anatakiwa aambiwe tu kuwa usuluhishi umeshafanyika, kuanzia sasa sina ugomvi na wewe... niliyokukosea nisamehe sitarudia tena, uliyonikosea nimekusamehe bila masharti yeyote... Kisha ampige mkewe hug, amkiss, amlale, alafu waende out kupata kitimoto. Kwishney...
sijakijua mkuu nielimishe
Ni cha kifamilia zaidi mkuu, sio vizuri kukiweka hapa. Kama utakutana mtu anamyemfahamu mtu anaitwa Balozi Ngaiza (sina uhakika kama bado yuko Msumbiji au keshastaafu)...
!
!
hakika. Kimsingi mwanaume ana nafasi mbili. Anaweza kuwa sehemu ya tatizo au anaweza kuwa sehemu ya utatuzi. Inategemea na jinsi anavyofanya maamuzi. Kwa hapa naona dalili kuwa huenda jamaa akawa sehemu ya tatizo
Kwa mantiki hiyo, yeye ndio sehemu ya suluhisho kama kweli analitaka!:israel:
Hbr wanajamii?,naomba ushauri ni wapi au nani ni sehem au mtu sahihi wa kuomba atusuruhishe kutoelewana na mke endapo sisi wenyewe tumeshindwa kufikia muafaka baada ya kujaribu kujisuhisha kwa zaidi ya mwaka bila mafanikio?