PreGE2025 Ugawaji wa majimbo mjadala mzito

PreGE2025 Ugawaji wa majimbo mjadala mzito

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,755
Reaction score
2,644
a0dc0d857798f198a6b3a78455ee474a.jpeg

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Jacobs Mwambegele

Wakati Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ikifunga mchakato wa kuchunguza na kugawa majimbo Machi 26, 2025, kumekuwa na mjadala kuhusu vigenzo vya ugawaji wa majimbo, kuyaongeza na kubadilisha majina.

INEC imepewa mamlaka ya kuchunguza mipaka na kugawa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Sheria Na.2 ya 2024 ya Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi kifungu cha 10(d).

Pia ibara ya 75 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inaipa INEC mamlaka ya kutekeleza jukumu hilo mara kwa mara na angalau kila baada ya miaka 10.

Mara ya mwisho tume iligawa majimbo ya uchaguzi mwaka 2015 ambapo majimbo mapya 25 yaliongezwa.

Kwa sasa Tanzania ina jumla ya majimbo ya uchaguzi 264 ambapo Bara kuna jumla ya majimbo 214 na visiwani Zanzibar yakiwa 50.

Akizungumza mkoani Morogoro Februari 26, Mwenyekiti wa INEC Jaji Jacobs Mwambegele alisema mchakato wa kugawa majimbo utaanza Februari 27, hadi Machi 26, 2025, akiwataka wadau kuzingatia vigezo.

Utaratibu

Kwa mujibu wa Kanuni ya 18(1) ya Kanuni za INEC za 2024, mapendekezo ya kugawa majimbo yanapaswa kujadiliwa na katika Kamati ya Ushauri ya Wilaya, ambayo mwenyekiti wake ni Mkuu wa wilaya na wajumbe ni pamoja na wabunge, madiwani na wakuu wa vitengo wa halmashauri.

“Hatua ya pili mapendekezo yawasilishwe kwa Katyibu Tawala wa Mkoa kwa ajili ya kuwasilishwa katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC).

“Tatu, Katibu Tawala wa Mkoa awasilishe mapendekezo INEC pamoja na viiambatanisho vyote,” alisema Jaji Mwambegele.

Vigezo

Kwa kuzingatia ibara ya 75(3 na 4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, ikisomwa pamoja na jedwali za tatu la kanuni za Tume ya Taifa ya Uchgauzi, kigezo cha kwanza ni wastani wa idadi ya watu, ambapo kwa mijini ni kuanzia watu 600,000 na vijijini ni kuanzia wastani wa watu 400,000.

Idadi hiyo ni kwa kufuata idadi iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kuzingatia matokeo ya Sensa ya Watu na makazi ya 2022.

Vigenzo vingine ni hali ya kiuchumi ya jimbo husika, ukubwa wa jimbo husika, mipaka ya utawala, jimbo moja kutokuwa ndani ya mikpaka ya halmashauri, mpangilio wa watu na makazi wa eneo husika.

Vingine ni uwezo wa ukumbi wa Bunge, idadi ya viti maalum vya wanawake, upatikanaji wa njia za mawasiliano na hali ya kijiografia ya eneo linalokusudiwa kugawanywa.

Majimbo yanayotarajiwa kugawanywa

Mpaka sasa majimbo yaliyofanya mijadala ya kugawanywa ni pamoja na Mbeya Mjini, ambapo Halmashauri ya Jiji la Mbeya imependekeza kuanza mchakato wa kuchunguza na kuligawa Jimbo hilo ili kupata jimbo jipya la Uyole, katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, 2025.

Jimbo hilo kwa sasa linaongozwa na Dk Tulia Ackson ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Muungano wa Mabunge Duniani (IPU).

Ukonga

Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) ikiongozwa Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila iliyoketi Machi 24, 2024 imepokea na kuridhia mapendekezo ya Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Ilala (DCC) ya kuligawa jimbo la Ukonga lililopo Wilaya ya Ilala kuwa majimbo mawili ambayo ni jimbo la Ukonga na jimbo Kivule.

Majimbo ya Tanga
Majimbo Tanga
Katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Tanga (RCC) kilichofanyika Machi 24, 2025 chini ya uenyekiti wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Burian, wajumbe kwa pamoja walikubaliana kuhusu ugawaji wa majimbo ya Kilindi, Muheza na Handeni Vijijini, kuwa na majimbo mawili kila moja katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Kwa mujibu wa mapendekezo hayo, Jimbo la Kilindi litagawanywa na kuongeza Jimbo jipya la Songe.

Handeni Vijijini litakuwa na majimbo mawili, Handeni na Kabuku, huku Muheza ikipendekezwa kuwa na majimbo mawili ya Muheza Mjini na Muheza Vijijini.

Balozi Batilda alifafanua kuwa majimbo ya Kilindi na Handeni Vijijini yamekidhi vigezo vya ugawaji kutokana na idadi ya watu na mazingira yao. Hata hivyo, kwa upande wa Muheza, idadi ya watu bado haijafikia vigezo vya Tume ya Uchaguzi vinavyohitaji jimbo kuwa na angalau wakazi 400,000.

Halmashauri ya Wilaya ya Muheza ina wakazi wapatao 250,000 na hata kwa makadirio ya ongezeko la watu, bado haifikii watu 300,000. Hivyo, kigezo kinachoweza kuzingatiwa ni idadi kubwa ya kata.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Muheza, Erasto Mhina alitoa hoja ya kuangalia upya mgawanyo wa jimbo hilo kwa sababu lina kata 37 na madiwani 50, wakiwamo wa viti maalum.

Hivi karibuni katika kikao cha DCC kilichoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Zainab Abdallah kilijadili mgawanyo wa maeneo mapya ya utawala kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Muheza yenye Jumla ya kata 37, kati ya hizo 17 ziunde Jimbo la Muheza Mjini na Kata 20 zilizosalia zitaunda Jimbo la Muheza Vijijini.

Kwela

Kwa upande mwingine, Kamati ya Ushauri (RCC) ya Mkoa wa Rukwa imeridhia kugawanywa kwa Jimbo la Uchaguzi la Kwela lililoko Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga.

Katika kikao chake cha Machi 14, 2025, Kamati hiyo imepokea kujadili na kuridhia kuendelea kwa mchakato wa kuligawa jimbo hilo ambalo kwa sasa linaongozwa na Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Deus Clement Sangu.

Chato, Busanda

Katika mchakato kama huo, kikao cha Kamisheni ya Ushauri ya Mkoa (RCC) wa Geita kimeridhia majimbo mawili ya uchaguzi ya Chato na Busanda yagawanywe kupata majimbo manne ili kuchagiza maendeleo.

Katibu Tawala Msaidizi, Mipango na Uratibu Mkoa wa Geita, Deodatus Kayango amewasilisha mapendekezo ya mkoa na kisha kuridhiwa na wajumbe wa kikao cha RCC kilichoketi maalum kwa ajili ya kujadili ajenda hiyo.

Solwa

Machi 11, 2025 Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, walijadili na kupitisha pendekezo la kugawa Jimbo la Solwa, kuwa na majimbo mawili ya uchaguzi ambayo ni Solwa na Itwangi.

Awali Ofisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Oscar Lupavila, akiwasilisha taarifa kwa Madiwani kwa niaba ya Mkurugenzi, amesema Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, ilitangaza kuligawa Jimbo la Solwa na kutoa vigezo vyake 10, ikiwamo idadi ya watu wanaokadiriwa kufikia 503,167 kufikia 2025.

Alisema Jimbo la Solwa likigawanywa, litakuwa na Watu 309,821 na Itwangi 193,346 na kwamba kati ya vijiji 126 na vitongoji 856, kuwa Solwa itakuwa na vijiji 68 na vitongoji 478,huku Itwangi itakuwa na vijiji 58 na vitongoji 378.

“Jimbo la Solwa kwa sasa lina ukubwa wa Kilomita za mraba 4,212, likigawanywa, Solwa itabaki kuwa na kilomita za mraba 2,573.29, na Jimbo la Itwangi, litakuwa na Kilomita za Mraba 1,638.71,” alisema Oscar.

Serengeti

Wajumbe wa kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mara (RCC) walipitisha Jimbo la Uchaguzi la Serengeti kugawanywa na kupata majimbo mawili ya uchaguzi ambapo majina ya majimbo yanayopendekezwa ni Serengeti Mashariki na Serengeti Magharibi.

Mkuu wa Mkoa wa Mara Evans Mtambi aliongoza kikao hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwekezaji ambapo aliwataka wakurugenzi wa Halmashauri kujiandaa kuweka mikakati ya ukusanyaji wa mapato ili kutekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi.

Mpaka sasa ni jimbo la Njombe pekee ndio limependekeza kubadilisha jina na kuitwa Njombe Kusini.

Serengeti
Maoni
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa amesema suala lisiwe tu kuongeza majimbo kwa ajili ya wabunge, bali hali ya uchumi pia iangaliwe, kwani wabunge hao watakuja kulipwa.

Ametaka kuwe na mjadala wa kitaifa ili wananchi watoe maoni kuhusu ugawaji huo wa majimbo.

“Inatafakarisha sana, kwani kwa sasa Watanzania hawahitaji msururu na lundo la viongozi badala yake hata hao waliopo ni wengi mno na tija yao haiaksi matokeo ya kazi zao,” amesema.

Akitoa mfano wa Dar es Salaam yenye majimbo 10, amesema vigezo havieleweki linapokuja suala la kijiografia.

“Dar es Salaam ina watu zaidi ya milioni sita, hivyo kuna majimbo yana watu zaidi ya 600,000. Je, idadi ya majimbo tuliyonayo inawiana na hivyo vigezo? Kuna mikoa ina majimbo mengi, lakini ukiangalia ya watu ni wachache.

“Kwa mfano Arusha ina watu zaidi ya milioni 2.5, lakini kijiografia ina eneo kubwa lakini majimbo machache. Zanzibar ina eneo dogo sana, lakini majimbo 50, kuna majimbo ya watu wachache kama watu 10,000.

“Naishauri tume yetu wakati huu inaendelea kufanya uchunguzi, tume iandae mjadala wa kitaifa, Watanzania watoe maoni kwamba vigezo gani tuaweza kuvitumia kugawa majimbo yetu,” amesema katika mahojiano na Jambo TV.

Akizungumzia mchakato huo, Wakili wa kujitegemea, William Maduhu amesema kuna baadhi ya majimbo yanastahili kugawanywa, akilitaja jimbo la Dodoma mjini.



Machi 26 ndio mwisho wa kamati kutoa mapendekezo ya kugawa majimbo.

“Jimbo la Dodoma Mjini ni kubwa na linaongoza kuliko majimbo yote nchini, lina kata 41.

“Lakini kwa Dar es Salaam, jimbo la Mbagala lina watu zaidi ya 700,000 kwa hiyo ukiligawa maana yake kila jimbo litakuwa na watu 350,000, hivyo idadi itakuwa haikidhi vigezo. Halafu kijiografia haikubali, kwa sababu lina kata chache,” amesema Maduhu kupitia televisheni ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Ameitaka INEC kutumia busara na kujiepusha na matamanio ya wanasiasa katika mchakato huo.

“Kumekuwa na tabia ya kupeana majimbo, yaani mtu anataka kugombea lakini haoni jimbo la kugombea, kwa hiyo jimbo linagawanywa, ili naye apate. Hizo ni sababu za kisiasa.

“Au unakuta jimbo lina kata 41 na linguine kata nane, lakini fedha za mfuko wa jimbo wanapewa sawa,” amesema.

Akizungumza Machi 2, 2025, katika mkutano wa CHADEMA na Jukwaa la Wahariri (TEF) jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu alikosoa mgawanyo wa majimbo 264 akisea hauzingatii usawa wa uwakilishi.

“Majimbo yamegawanywa kwa upendeleo mkubwa kati ya Tanganyika na Zanzibar, miji na vijijini, na hata mikoa kwa mikoa. Hili linavuruga uwakilishi wa wananchi,” alisema Lissu.

Alihoji kwa nini idadi ya watu haizingatiwi katika mgawanyo huo, akitoa mfano wa Jimbo la Temeke lenye wapiga kura 478,000, linalowakilishwa na mbunge mmoja, huku majimbo yote 50 ya Zanzibar yenye wapiga kura 566,000 yakitoa wabunge 50.

Lissu alisisitiza kuwa mfumo huu unahitaji marekebisho ili kuhakikisha haki na usawa katika uwakilishi wa wananchi bungeni.

"Mfumo wa Majimbo umevurugwa hauna usawa. Kuna mbunge anachaguliwa na watu 1,000 na mwingine watu 132,000," Tundu Lissu
 
Hili wala halistahili kwa sasa wakati huu uchumi wetu hauko sawa sana mnaongeza gharama za majimbo tena.
 
KIla mkoa wabunge wawili..wote wa kuchaguliwa..mmoja wa mkoa mwingine wa makundi maalum..period..

Now tuna madiwani wa kutosha na miundo mbinu mizuri kama barabara+ cmu bila kusahau vyombo habari

La mwisho hizo hela za hao wabunge wa kuongezwa,zielekezwe kwenye shughuli za maendeleo..
 
Kinachoniuma zaidi kwa ngazi za chini huku wanaoshughulikia mgawanyo wa majimbo ni wanachama wa CCM, hapo ni kuongeza tu fursa zao na si kwa ajili ya maendeleo kwa wananchi.
 
CCM kila uchaguzi ukikaribia wanahangaika na majimbo, yaani namna ya kuigawana Tanganyika bila ridhaa yetu.
 
Watoto wa masikin wanaambiwa waende veta lakin pesa za kulipa watu mil 9-15 zipo

Ila wanasiasa wa afrika mungu atakuja wafanya kitu kibaya
 
Back
Top Bottom