Kwa nini iwe kosa jinai mtu kuwa shoga? Sielewi kabisa mimi.
Not only that because the anti-homosexuality bill also makes it a crime punishable by a prison sentence not to report gay people.
Uganda imepitisha mswada unaopinga mapenzi ya jinsia moja.
Iwapo Rais Yoweri Museveni ataidhinisha sheria hiyo inamaanisha atakayepatkana na hatia atahukumiwa kifungo cha maisha gerezani.
Mswaada huo uliopitishwa na bunge siku ya Ijumaa halikadhalika inasema mtu yeyote aliye na taarifa za watu wanoshiriki mapenzi ya jinsia moja na kushindwa kuripoti habari hizo kwa maafisa wa polisi atafungwa gerezeni maisha.
Wakati hu huo bunge hilo hilo la Uganda siku ya Alhamisi liliidhinisha mswaada unaopiga marufuku maonyesho ya picha za chafu.
Mswada huo unaharamisha kitu chochote kitakachoonyesha sehemu nyeti kama vile matiti, mapaja, makalio au tabia yoyote inayozua uchu wa mapenzi.
Kulingana na mswada huo, sheria iliyopo sasa kuhusu picha chafu haihusu zaidi picha hizo bali linahusu uchapishaji ,mawasiliano, taarifa , burudani, maonyesho katika kumbi za kuigizia, miziki inyochezwa katika vyombo vya habari, densi, sanaa, mitindo na picha za runinga.
Mapema mwaka huu Waziri wa maadili wa Uganda, Simon Lokodo, alipendekeza kuwa mwanamke yeyote anayevalia nguo ambayo inafika juu ya magoti anatakiwa kukamtwa na kuadhibiwa kisheria.
Mswada huo unahitaji kuidhinishwa na Rais kabla ya kufanywa sheria.
Uganda ni nchi inayoshikilia mawazo ya kihafidhina yaani isiyopendelea mageuzi katika mawazo na inaandaa sheria ya kuwaadhibu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja ikijumuisha hukumu ya kifo katika baadhi ya kesi.
SOURCE: BBC Swahili
Lakini mkuu lengo kuu la sheria si kutoa haki kama wengi wanavyoaminishwa, lengo kuu la sheria ni kulinda utu wa mtu , halafu kutoa haki ni second target.Asigwa katika paragraph yako ya pili kama watapitisha hivyo majanga! Na hiyo sheria itakua kinyume na principle za law! Just imagine, umegundua mwanao ndio anafanya hivyo!
Hivi itamaanisha wewe uliejua hiyo kitu unapenda iwe hivyo?
Nadhani wabunge wa Uganda na raisi wao if akikubali huo mswada itabidi wanuswe midomo! Otherwise waspecify mazingira ya hiyo kitu!
And refers sheria haipo kwa niaba ya kukandamiza watu, refers John lock, Montesque na Plato!
...1
Lakini mkuu lengo kuu la sheria si kutoa haki kama wengi wanavyoaminishwa, lengo kuu la sheria ni kulinda utu wa mtu , halafu kutoa haki ni second target.
...2
Sasa kama utu wa binadamu unadhalilishwa kwa misingi ya kudai haki ambazo bado ziko challengeable mahakamani unafikiri kuna haja ya kumlaumu Museveni??
Kweli kuna haja ya kubadili hicho kipengele cha anayekuwa na taarifa lakini asiripoti polisi, angalau adhabu inaweza kuwa faini au miaka kama mitano hivi......1
Asigwa hapo kuna mjadala mrefu sana!
Tupaache tu!
...2
Mu7 atalaumika if akisign hiko kipengel
e cha mswada kinachosema "yoyote atakaejua hizo habari na kushindwa kuripoti!"
hapo ndio kunautata!