Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi wamefunga mipaka ila Tanzania ruksa. Sijui tunatafuta nini au hatujali raia? Kunawa mikono ndio kinga?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Lengo la Rais Magufuli na serikali yake mpaka sasa sijaelewa na nchi hii ni tajiri tunaogopa nini kufunga mipaka kukabiliana na Corona?

Nchi jirani wamepiga marufuku kuingia wala kutoka katika nchi zao sie kimya.

Kwa mfano Museveni yeye kapata raia mmoja kaambukizwa keshachukua hatua.

Ila cha ajabu nashangaa Tanzania tunaita viongozi wa dini eti waombee taifa, hivi kule Roma kanisa lilimo anzia ndio wamekufa kuliko wachina hawana viongozi wa dini? Kwani hawakuombea Italia wapone?

China aliweza kujenga hospitali ndani ya siku 7 sie tunakalia ngonjera za kunawa mikono
 
Sisi sio waoga kama kunguru.

Naunga mkono hoja na hapa ndipo ninapompendea rais Magufuli, kwenye ukweli, hakopeshi.

Sio tuu hakuna aliyekufa kwa Corona bali hakuna Mtanzania aliyeambukizwa Corona akiwa nchini, hivyo Corona Bongo haiambukiziki, huku nikisisitiza Corona ni ugonjwa wa ulaya na nchi za baridi, sio tropical disease
P
 
Boss leo kasema corona isitutishe
Watu wana kufa kwa ukimwi, kifua kikuu, kansa na hata ajali. Corona haija ua mtu hata mmoja hapa Tanzania. Hofu ya nini? Msi tutishe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zanzibar wamezuia wageni.... au unazungumzia Tanzania ipi?
 

Anataka corona iingie "KWERI KWERI" sio "KORONA ya KINA SALAMA NA FATUMA" tusifanye uchaguzi October 2020.
 
Sometimes ni vizuri kuweka akiba ya Maneno na pia uje China walijitahidi kuficha hali halisi ya ugonjwa ila ilifika hatua wakasalimu amri.
 
kama majirani zetu wamefunga mipaka na sisi baadhi yetu ya mipaka imeshajifunga hakuna Tatizo ila juzi Kagere karudi Rwanda sijui kapitia mpaka gani?
 
Hapo ndipo napompendea Rais Magufuli. Kiongozi anayeweza kutumia akili yake mwenyewe kufikiri. Wengi wa viongozi wa Afrika naona wanareact tu kama robots tu kwenye corona.
 
kama majirani zetu wamefunga mipaka na sisi baadhi yetu ya mipaka imeshajifunga hakuna Tatizo ila juzi Kagere karudi Rwanda sijui kapitia mpaka gani?

Tunahitaji kuwalazimisha viongozi wetu kufunga mipaka. Waache kuchezea uhai wa wananchi kitoto. Janga la Corona virus si la mchezo. Likizuka hapa nchini hatuna uwezo wowote wa kupambana nao. Tuache ushamba na ulimbukeni wa kiuongozi kwenye uhai wa raia.
 
Acha kutisha watu funga nyumba yako
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…