Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi wamefunga mipaka ila Tanzania ruksa. Sijui tunatafuta nini au hatujali raia? Kunawa mikono ndio kinga?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,568
2,000
Lengo la Rais Magufuli na serikali yake mpaka sasa sijaelewa na nchi hii ni tajiri tunaogopa nini kufunga mipaka kukabiliana na Corona?

Nchi jirani wamepiga marufuku kuingia wala kutoka katika nchi zao sie kimya.

Kwa mfano Museveni yeye kapata raia mmoja kaambukizwa keshachukua hatua.

Ila cha ajabu nashangaa Tanzania tunaita viongozi wa dini eti waombee taifa, hivi kule Roma kanisa lilimo anzia ndio wamekufa kuliko wachina hawana viongozi wa dini? Kwani hawakuombea Italia wapone?

China aliweza kujenga hospitali ndani ya siku 7 sie tunakalia ngonjera za kunawa mikono
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,968
2,000
Sisi sio waoga kama kunguru.

“#Corona mpaka sasa hivi haijaua mtu hata mmoja hapa #Tanzania…lakini tunatishana sana…ninaanza kupata wasiwasi kwamba inafika mahali mpaka watu tumeanza kumsahau Mungu,” - Rais Magufuli alipohudhuria Ibada ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Paulo wa Msalaba, Jimbo Kuu la Jimbo Kuu Katoliki la #Dodoma.

RAIS MAGUFULI: IMEFIKIA MAHALI WATU WANAOGOPA HATA KWENDA KANISANI

“Imefikia mahali watu wanaogopa hata kwenda kanisani…msikitini wakihofia watapata #Corona.

Ninaweza nikafikiria kwa mawazo yangu madogo kwamba katika kipindi ambacho shetani ameutawala ulimwengu ni kipindi hiki,” – Rais Magufuli.

RAIS MAGUFULI ATAKA WATANZANIA WASITISHANE NA CORONA

“Watu tusitishane, tunatishana mno. Niwaombe ndugu Wakristo na Watanzania kwa ujumla wa Madhehebu yote, huu ndio wakati mzuri sana wa kumtegemea Mungu kuliko wakati wote, tuendelee kuchapa kazi, tuendelee kuujenga uchumi wetu, hatuwezi kusalimu amri kwa ugonjwa huu wa Corona na kushindwa kumtegemea Mungu na tukashindwa kuendeleza uchumi wetu” - Rais Magufuli.

#CoronaVirus #CoronaOutbreak #MagufuliCorona #CoronaUchumi #CoronaTanzania
Naunga mkono hoja na hapa ndipo ninapompendea rais Magufuli, kwenye ukweli, hakopeshi.

Sio tuu hakuna aliyekufa kwa Corona bali hakuna Mtanzania aliyeambukizwa Corona akiwa nchini, hivyo Corona Bongo haiambukiziki, huku nikisisitiza Corona ni ugonjwa wa ulaya na nchi za baridi, sio tropical disease
P
 
LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
6,398
2,000
Lengo la Magufuli na serikalo yake mpaka sasa sijaelewa ma nchi hii ni tajiri tunaogopa nini kufinga mipaka kukabiliana na corona?

Nji jirani wamwpiga marufuku kuingia wala kutoka katika nchi zao sie kimyaa.

Kwa mfano mseven yeye kapata raia mmoja kaambukizwa keshachukua hatua.

Ila cha ajabu nashangaa tanzania tunaita viongozi wa dini eti waombee taifa, ivi kule Roma kanisa lilimo anzia ndio wamekufa kuliko wachina hawana viongozi wa dini? Kwa n hawakuombea Italia wapone?

China aliweza kujenga hospital ndani ya siku 7 sie tunakalia ngonjera za kunawa mikono
Boss leo kasema corona isitutishe
Watu wana kufa kwa ukimwi, kifua kikuu, kansa na hata ajali. Corona haija ua mtu hata mmoja hapa Tanzania. Hofu ya nini? Msi tutishe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
38,741
2,000
Lengo la Magufuli na serikalo yake mpaka sasa sijaelewa ma nchi hii ni tajiri tunaogopa nini kufinga mipaka kukabiliana na corona?

Nji jirani wamwpiga marufuku kuingia wala kutoka katika nchi zao sie kimyaa.

Kwa mfano mseven yeye kapata raia mmoja kaambukizwa keshachukua hatua.

Ila cha ajabu nashangaa tanzania tunaita viongozi wa dini eti waombee taifa, ivi kule Roma kanisa lilimo anzia ndio wamekufa kuliko wachina hawana viongozi wa dini? Kwa n hawakuombea Italia wapone?

China aliweza kujenga hospital ndani ya siku 7 sie tunakalia ngonjera za kunawa mikono
Zanzibar wamezuia wageni.... au unazungumzia Tanzania ipi?
 
Savimbi Jr

JF-Expert Member
Sep 23, 2011
6,736
2,000
Lengo la Magufuli na serikalo yake mpaka sasa sijaelewa ma nchi hii ni tajiri tunaogopa nini kufinga mipaka kukabiliana na corona?

Nji jirani wamwpiga marufuku kuingia wala kutoka katika nchi zao sie kimyaa.

Kwa mfano mseven yeye kapata raia mmoja kaambukizwa keshachukua hatua.

Ila cha ajabu nashangaa tanzania tunaita viongozi wa dini eti waombee taifa, ivi kule Roma kanisa lilimo anzia ndio wamekufa kuliko wachina hawana viongozi wa dini? Kwa n hawakuombea Italia wapone?

China aliweza kujenga hospital ndani ya siku 7 sie tunakalia ngonjera za kunawa mikono

Anataka corona iingie "KWERI KWERI" sio "KORONA ya KINA SALAMA NA FATUMA" tusifanye uchaguzi October 2020.
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,888
2,000
Sisi sio waoga kama kunguru.

Naunga mkono hoja na hapa ndipo ninapompendea rais Magufuli, kwenye ukweli, hakopeshi.

Sio tuu hakuna aliyekufa kwa Corona bali hakuna Mtanzania aliyeambukizwa Corona akiwa nchini, hivyo Corona Bongo haiambukiziki, huku nikisisitiza Corona ni ugonjwa wa ulaya na nchi za baridi, sio tropical disease
P
Sometimes ni vizuri kuweka akiba ya Maneno na pia uje China walijitahidi kuficha hali halisi ya ugonjwa ila ilifika hatua wakasalimu amri.
 
rodrick alexander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
8,323
2,000
kama majirani zetu wamefunga mipaka na sisi baadhi yetu ya mipaka imeshajifunga hakuna Tatizo ila juzi Kagere karudi Rwanda sijui kapitia mpaka gani?
 
zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
668
1,000
Hapo ndipo napompendea Rais Magufuli. Kiongozi anayeweza kutumia akili yake mwenyewe kufikiri. Wengi wa viongozi wa Afrika naona wanareact tu kama robots tu kwenye corona.
 
share

JF-Expert Member
Nov 22, 2008
5,489
2,000
kama majirani zetu wamefunga mipaka na sisi baadhi yetu ya mipaka imeshajifunga hakuna Tatizo ila juzi Kagere karudi Rwanda sijui kapitia mpaka gani?

Tunahitaji kuwalazimisha viongozi wetu kufunga mipaka. Waache kuchezea uhai wa wananchi kitoto. Janga la Corona virus si la mchezo. Likizuka hapa nchini hatuna uwezo wowote wa kupambana nao. Tuache ushamba na ulimbukeni wa kiuongozi kwenye uhai wa raia.
 
STDVII

JF-Expert Member
Nov 24, 2014
1,588
2,000
Acha kutisha watu funga nyumba yako
Tunahitaji kuwalazimisha viongozi wetu kufunga mipaka. Waache kuchezea uhai wa wananchi kitoto. Janga la Corona virus si la mchezo. Likizuka hapa nchini hatuna uwezo wowote wa kupambana nao. Tuache ushamba na ulimbukeni wa kiuongozi kwenye uhai wa raia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom