Wana JF,
Nimeona mm pia nitoe testimonial kwa faida ya wajasiriamali wanaopenda kilimo na ufugaji.
Ndoto yangu imekuwa kutafuta ujasiriamali utakaoniwezesha kuachana na ajira at 40yrs.Baada ya kujaribu biashara mbalimbali nikagundua kuwa faida zilizopo kwenye kilimo na ufugaji ni kubwa mno especially kama una kamtaji ka kuanzia kapo.Nikaanza kutafuta mashamba.Nikapata kadhaa ila hili la Maseyu ndilo hasa linazaa matunda.kwa wale wanajua morogoro road,hicho kijiji kipo baada ya bwawani au km6 kabla ya mikese.Shamba lipo km1.5 toka barabarani.Nilinunua eka 100 mwaka 2011.Immediately nikaanza kufyeka na kung'oa visiki.Nikalima eka10 za mahindi na alizeti mwishoni 2012.Nililima eka 2 za tikiti maji.mazao yanastawi si mchezo.masika ya 2013 nikalima eka 20 za alizeti na mahindi.pia nikaanzisha mradi wa nguruwe.
Nilianza na nguruwe 8 jike na dume mmoja.sasa nina nguruwe kama 70 hv.Nilipata changamoto kidogo,nguruwe watatu walikufa.kwa changamoto hizo nimepata uzoefu mkubwa. Mambo mengi kama kuchoma chanjo na kutibu baadhi ya magonjwa naweza kufanya mwenyewe kwa maana madaktari nao ni changamoto.nategemea kuanza kuuza nguruwe wakubwa by April.wadogo nauza though soko lake sio kubwa sana.
Pamoja na upunyufu wa mvuA mazao yangu ya vule yamekomaa.nna tikiti kama eka10 na mahindi kama eka25.
Nextmonth nategemea kulima eka kama 70 hv.nataka kulima mahindi,alizeti,ufuta,mtama na maboga.vyote kwa biashara na chakula ya mifugo yangu.
Nataka niweze kuuza nguruwe 20 kila mwezi by this year.
Mwaka jana nimevuna zaidi ya gunia 200 za mahindi na 150 za alizeti.fuso 2 za tikiti maji.Cha zaidi nimetoa ajira kwa vijana kazaa
Tatizo la maji shambani nimetatua last year kwa ku design bwawa na matank cheap.
Karibuni wajasiriamali,future ipo kwenye kilimo.unauza mazao yako hamna mtu anakuuliza kodi! Hahaa
Maelezo yote ya mtaji kesha sema someni thread hizi kabla ya kuuliza. Hata hivyo suala la magunia 200 au 150 si kitu cha stusha kwani mahindi kimsingi huchukua takribani siku 90 unavuna! Kama alipanda ekari kuimi hayo magunia 150 hadi 200 ni cha mtoto Mr!Heka 100 ulinunua kwa sh ngapi? Ulianza lini kufuga nguruwe au 9 na mpka leo wapo 70? Maelezo mengi hayajakamilika gunia 200 na 150. Ulilima lini?
Ahsante mzee mkaruka.Maelezo yote ya mtaji kesha sema someni thread hizi kabla ya kuuliza. Hata hivyo suala la magunia 200 au 150 si kitu cha stusha kwani mahindi kimsingi huchukua takribani siku 90 unavuna! Kama alipanda ekari kuimi hayo magunia 150 hadi 200 ni cha mtoto Mr!
mKUU Mbimbinho,
ahsante.
1. sehemu ninayofugia ni shambani mbali kidogo na makazi ya watu. Usalama upo kwani kuna vijana pale wanaangalia
2. Nguruwe mkubwa anauzwa kuanzia 200,000-400,000 inategemea ana uzito gani. Nguruwe mdogo alietoka kuachishwa anauzwa kwa shs.30,000-40,000 inategemea na uzito
3. Nguruwe huchukua miezi 6-8 kufika uzito wa kuuzwa .inategemea na matunzo
4. Ufuta una stawi sana! Masika hii nategemea kulima eka10 za ufuta.
Nashauri kama upo interested tembelea wafugaji na wakulima walio karibu kupata uzoefu.
Ok.mi sijawahi lima ufuta ila jirani yangu alilima mwaka jana.Asante sana mkuu MalafyaleP
Mkuu kama nitakusumbua tena, kwa sasa mimi target yangu nni kulima Ufuta mwakani, hivo kwa sasa hivi nafanya kautafiti fulani hivi, then later on after a year or two ndo nitarudi kufuga.
Tafadhali naomba nisaidie kwenye ufuta, faida, soko na changamoto za kilimo hiki sina uzoefu wa kutosha na pia ghrama zake za uzalishaji kwa eka. Kwa sasa nina shamba kama ekari 40 maeneo ya vigwaza karibu na chalinze, hopefully ardhi hazitofautiani sana.
Mkuu nimevutiwa na uzi wako.
Nami nipo kwenye hz harakt bado nakusanya nguvu.
Hivi ufuta kwa heka unaweza vuna gunia ngap kwa wastani?nipo dodoma je maeneo gani ufuta unakubali?na mahitaji yake ya hali ya hewa yapoje na gharama zake kwa heka ni kiasi gani??
Ok.mi sijawahi lima ufuta ila jirani yangu alilima mwaka jana.
Ufuta ni high value crop.kwa kilo inaweza fika 3500 na wanakufuata shambani.
Ufuta unahimili vizuri uchache wa mvua na kwa heka ukipata mbegu nzuri kama lindi unaweza pata kilo 1000.
Unahitaji kupiga dawa wadudu waharibifu.
Changamoto kubwa ni uvunaji.usipojipanga vizuri sehemu kubwa inapotea shambani.unahitaji kujua wakati muafaka wa kuvuna .
Nimeona kuna threads kuhusu ufuta,jaribu ku peruse.
Je huko vigwaza wanachi wanalima nn? Kama kuna mazao wanalima masika,ufuta utakuwa unakubali maana maeneo yote ya pwani ufuta unastawi
Mimi nililimisha Handeni mwaka jana kila ekari moja nikapata kilo 400 (@3,200/=)
Mkuu kwa sasa bado unaendelea kulima?? na hiyo bei ni bei ya shambani or ya sokoni?
Vipi kuna changamoto gani ulizopitia??
Vipi unafikiri ungeweza kuvuna zaidi ya hizo kilo 400 kwa Ekari moja???
Samahani mkuu kwa maswali, but tuvumiliane mkuu.
Wana JF,
Nimeona mm pia nitoe testimonial kwa faida ya wajasiriamali wanaopenda kilimo na ufugaji.
Ndoto yangu imekuwa kutafuta ujasiriamali utakaoniwezesha kuachana na ajira at 40yrs.Baada ya kujaribu biashara mbalimbali nikagundua kuwa faida zilizopo kwenye kilimo na ufugaji ni kubwa mno especially kama una kamtaji ka kuanzia kapo.Nikaanza kutafuta mashamba.Nikapata kadhaa ila hili la Maseyu ndilo hasa linazaa matunda.kwa wale wanajua morogoro road,hicho kijiji kipo baada ya bwawani au km6 kabla ya mikese.Shamba lipo km1.5 toka barabarani.Nilinunua eka 100 mwaka 2011.Immediately nikaanza kufyeka na kung'oa visiki.Nikalima eka10 za mahindi na alizeti mwishoni 2012.Nililima eka 2 za tikiti maji.mazao yanastawi si mchezo.masika ya 2013 nikalima eka 20 za alizeti na mahindi.pia nikaanzisha mradi wa nguruwe.
Nilianza na nguruwe 8 jike na dume mmoja.sasa nina nguruwe kama 70 hv.Nilipata changamoto kidogo,nguruwe watatu walikufa.kwa changamoto hizo nimepata uzoefu mkubwa. Mambo mengi kama kuchoma chanjo na kutibu baadhi ya magonjwa naweza kufanya mwenyewe kwa maana madaktari nao ni changamoto.nategemea kuanza kuuza nguruwe wakubwa by April.wadogo nauza though soko lake sio kubwa sana.
Pamoja na upunyufu wa mvuA mazao yangu ya vule yamekomaa.nna tikiti kama eka10 na mahindi kama eka25.
Nextmonth nategemea kulima eka kama 70 hv.nataka kulima mahindi,alizeti,ufuta,mtama na maboga.vyote kwa biashara na chakula ya mifugo yangu.
Nataka niweze kuuza nguruwe 20 kila mwezi by this year.
Mwaka jana nimevuna zaidi ya gunia 200 za mahindi na 150 za alizeti.fuso 2 za tikiti maji.Cha zaidi nimetoa ajira kwa vijana kazaa
Tatizo la maji shambani nimetatua last year kwa ku design bwawa na matank cheap.
Karibuni wajasiriamali,future ipo kwenye kilimo.unauza mazao yako hamna mtu anakuuliza kodi! Hahaa
Mwaka jana nililimisha eka 5 tu mwaka huu nalimisha 50. changamoto ni nyingi muhimu zikiwa:
[*=1]Kuyajua majira ya kilimo vizuri
[*=1]Aina ya mbegu. Mwaka huu nimepata mbegu toka Mtwara ambayo ni nzuri kidogo.
[*=1]Watu wa kule wakorofi sana lazima waingie shamba kukusaidia kuvuna(kwa kukuibia)
[*=1]Muda wa usimamizi na ufuatiliaji.
[*=1]​Mvua isiyokuwa ya uhakika