Ufuatiliaji unaoheshimu usawa: Vyombo vya dola vifuate SOP

Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,503
2,378
Kwenye nchi zenye historia ya ubaguzi wa rangi kama Marekani mara nyingi raia weusi wanalalamika kwamba mtoto mweusi akipotea au akitekwa suala lao huwa halivaliwi njuga kwa uzito unaostahili kwenye media, matangazo ya polisi na matamko ya viongozi. Lakini mtoto wa kizungu akipotea vyombo vya dola vinashusha jehanam mtaani, "all hell breaks loose."

Standard Operating Procedure huwa zinatengenezwa kwa makusudi ya kurahisisha uchunguzi kutokana na uzoefu uliopatikana lakini pia kuepuka tatizo la vyombo vya dola kuonekana vina upendeleo. Na hufuatwa kikamilifu katika kila hatua baada ya matukio ikiwemo hata jinsi ya kutoa matamko kwa umma wakati wa uchunguzi, na kuonyesha ufuatiliaji ulio sawa kwa kila faili.

Wananchi wanachunwa ngozi, wanapotea, wanatekwa, mbona hatusikii tukio moja hilo hilo linatolewa matamko na RPC, Waziri wa Mambo ya Ndani na Mkuu wa Mkoa, kiasi cha kuahidi "watapatikana by Sunday"? Wengine wanaopotea na kupotezwa kimya kimya wao ni mbuzi? Hili sio tatizo jipya. Jeshi la Polisi wanapaswa wawe wamesha devise hizo SOPs na zifuatwe kikamilifu.

Ninajua viongozi wetu wa vyombo vya dola wana exposure na mambo haya, wameishi, kusoma au kufanya kazi ndani na nje ya nchi, ikiwemo taasisi kama ya Interpol ambayo hufanya mambo yake kwa kufuata taratibu za SOPs. Ni vema wakaleta nyumbani uzoefu wa practices kama hizo.

Raia wote wa nchi hii wana thamani ya utu sawa. Na yeyote anaeopotea au kutekwa anastahili msukumo ulio sawa kutoka kwa viongozi husika na pia vyombo vya ulinzi na usalama. Sio wahanga wa tasnia moja tu ya watu maarufu.
 
Back
Top Bottom