Nimechoka kushanagaa!..sasa hivi imeshakuwa ni jambo la kawaida tu watu kuhujumu pesa za walipakodi, na hakuna anayejali kwani kila kukicha utasikia mara kuna mabilioni uswiss, mara rada yetu mpya imeharibika, mara utasikia kodi zetu zinampeleka mwenyenyumba kubembea jamaica, wakati mwingine kaenda kula tende. Haya yote yanaanza kuzoeleka masikioni mwetu.
Mytake: Tuongeze elimu ya uraia kwa wananchi wetu ili tuhakikishe 2015 wapigakura wanajitokeza na kupiga kura makini.
Mungu ibariki Tanzania