Ufisadi wa viongozi wa ngazi za juu unaathiri sana wananchi wa vijijini

Kwamhuzi

JF-Expert Member
Nov 15, 2014
1,762
400
Dakwa ni kijiji ambacho kiko mkoa wa Morogoro.Ingawa ni kijiji kwa sasa, lakini hatimaye kitakuwa sehemu ya mji mdogo wa DAKAWA SOKOINE kwa vile kiko kwenye eneo ambapo mji huo mdogo unapaswa kuwepo.Kwa bahati nzuri kijiji hiki kilpata mradi wa maji,lakini kwa sababu ya usimamizi mbovu katika ujenzi wake, malengo yaliyokusudiwa hayakufikiwa.Mimi sio mtaalam wa maji,,lakini hata katika ufahamu mdogo nilio nao mradi una matatizo katika ujenzi wake kwa hiyo upatikanaji wa maji umekuwa wa matatizo katika maeneo mengi.Kama hii haitoshi,uongozi nao umekuwa tatizo.Uongozi wa mwanzo wa mradi na hata wa pili ulijikita katika ulaji wa fedha,na hata wananchi walipolalamika hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa.inashangaza sana kwa vile hata Mkurugenzi wa maendeleo wa Wilaya wananchi walipomuona alionyesha kujali lakini hakuna alilofanya la maana kuwasaidia wananchi kutokana na adha ya maji waliyo nayo ambayo kwa kweli inatokana na matumizi mabaya ya fedha za ankara. Ni kweli amebadilisha uongozi wa awali, lakini matatizo yamebaki yale yale na hakuna anayewajibishwa.Juu kumeoza kumeambukiza chini.Ni lazima Watanzania tujenge mazoea ya kuwajibika na kuwajibishana bila kulindana kuanzia juu.Vinginevyo nchi itaangamia.Watumishi wa chini wanakosa uwajibikaji kwa vile viongozi wa juu hawawajibiki kabisa.Hawawezi kuwawajibisha kwa vile wao wenyewe wameoza.Hapana,hatuwezi kuendelea hivi.Tunatoa mfano gani kwa vizazi vijavyo?Tanzania imekuwa kichekesho kwa mataifa mengine,Radar,EPA,RICHMOND,Tegeta,ESCROW na mengine mengi ambayo hatuyajui.Nadhani tufike mahali tuseme inatosha.
 
Back
Top Bottom