Ufisadi na Ugonjwa dhidi ya Edward Lowassa

Ufisadi na Ugonjwa dhidi ya Edward Lowassa

Shondola

Member
Joined
Apr 2, 2014
Posts
95
Reaction score
58
Ndugu wanaJF na wapenzi wasomaji Salaam;Kuna mengi nimetafakari na nikapata majibu kuntu yaliyonilazimisha kuchukua kalamu na kushirikiana na Watanzania ambao wengi wao sasa hivi wamekuwa guru katika kutafiti na katika kusoma na hivyo kwao hoja ndizo zenye mashiko na hujibiwa kwa hoja vile vile.

Binafsi kwanza nikiri kuwa ndani na nje ya CCM bado Edward Lowassa kwangu ataendelea kubaki kama "Role Model" na mtu anayestahili kuongoza Taifa hili kama ambavyo Watanzania walio wengi wanavyomwombea kila kukicha ili ndoto yake itimie katika Safari yake ya Matumaini. Hivyo niandikapo haya najiweka wazi kupokea changamoto zozote zile ila nami niwashauri kuwa siku zote Ukweli ndio utakao mweka mtu Huru.

Nakumbuka EL Safari yake hii aliyoianzisha alikiri kuwa ni Safari iliyojaa vikwazo vingi, mafuriko, miiba, kashfa, kejeli, vita na mambo yafananayo na hayo na huwa huyu bwana amejaliwa uwezo wa pekee kama Nabii (He is a Visionary Leader) manake hayo aliyoyasema hata mwezi haujapita tumeshuhudia kilichofanywa na Kamati mbali mbali ndani ya Chama chao ikiwemo Kamati inayooitwa ya Mangula na baadae Kamati Kuu chini ya Mwamvuli wa Kumpunguza kasi lakini ndo kwanza kama vile wameongeza Petroli kwenye Moto. Huwezi zuia mafuriko kwa viganja viwili.

Muktadha wa andiko hili kwa leo si kutaka ama kuelezea au kupingana na Kamati Kuu ya CCM bali ni kuweka bayana na kufafanua baadhi ya mambo ambayo wananchi wengi wameona kama ni kikwazo EL kufikia ndoto zake………. Sasa naanza japo kwa ufupi sana.

RICHMOND Pamoja na kuwa hili swala limekuwa kama nyimbo zisizo na chorus na pamoja na kuwa EL mwenyewe alikwishawahi kulitolea ufafanuzi japo ni kwenye vikao vyao vya kichama kuna baadhi ya mambo ambayo ni lazma yawe wazi.

Tarehe 15.02.2008 kwa mujibu wa taarifa rasmi za majadiliano ya Bunge (Hansard) Dr, Harrison Mwakiembe (Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume Teule) wakati akihitimisha hoja ya Kamati yake alisema (Nanukuu);

"Mheshimiwa Spika ninaomba nianze na utangulizi mfupi na rahisi; uwajibikaji kwa viongozi waandamizi katika nchi zinzolinda na kuenzi demokrasi kama vile Tanzania una sura mbili; Sura ya kwanza kiongozi anawajibika kwa makosa yake mwenyewe ya kiutendaji. Kiongozi anafanya maamuzi mabaya pengine kwa kishawishi cha pesa, maamuzi yake yakaleta hasara au kiongozi ameshindwa kutoa ushauri mzuri kama kiongozi kwa kukiuka kanuni, kukiuka utaratibu na kadhalika, matatizo yakatokea, ANAWAJIBIKA.Sasa sura hii ya uwajibikaji inahusisha uvunjwaji wa maadili, kanuni, sheria, miiko ya uongozi na kadhalika.

Chini ya uwajibikaji wa aina hii, kiongozi anaweza akashitakiwa, akaadhibiwa mbali na kuachia ngazi. Nitarejea kwenye sura hii hivi punde. Suala la msingi hapa ni kuwa, kuna element ya adhaby katika sura hii ya kwanza.
Sura ya pilli; kiongozi anawajibika kwa makosa ambayo si yake moja kwa moja ila yaliyofanywa na watendaji chini yake. Kitendo cha kuwajibika kwa aina hii kunaijengea Serikali au taasisi heshima na imani ya pekee katika jamii na kunatoa picha ya kwamba, uongozi unajali na unaielewa tatizo kwa kubeba lawama wao wenyewe (MAKOFI).

Mheshimiwa Spika, katika suala hili la Richmond viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini na Waziri Mkuu walikuwa wanakabiliwa na Uwajibikaji wa aina hizo mbili;Kwanza, uwajibikaji unaotokana na makosa ya viongozi wenyewe katika maamuzi yao maelekezo yao maagizo yao na kadhalika. Mawaziri wote wawili wa Nishati na Madini aliyetangulia na aliyefuata baadaye, Katibu Mkuu na Kamishna wa Nishati, wote tukawaona wana makosa ya moja kwa moja waliyoyafanya wao kwa njia moja au nyingine.

Kwa kuwa uwajibikaji wa aina hii unatokana na ukiukwaji wa kanuni, taratibu, maadili, sheria na kadhalika, Kamati Teule ikahakikisha inawahoji wote ili kusikia their side of the story kabla ya kutoa pendekezo la kuwawajibisha kwa makosa waliyoyafanya, Ndiyo maana baada yakuwahoji tumependekeza hatua za kuchukuliwa dhidi yao.Hali HAIKUWA hivyo kwa Waziri Mkuu;

Kamati Teule ilikuwa na ushahidi wa mawasiliano ya karibu kati ya Waziri Mkuu na Uongozi wa Wizara. Ushahidi huo haukutosha kwa uwajibikaji wa sura ile ya kwanza wa kiongozi kukutwa na makosa ya moja kwa moja, aliyoyafanya yeye mwenyewe kwa njia moja au nyingine, lakini ushahidi huo ulitosha kwa uwajibikaji wa sura ya pili, ambao hauhitaji mahojiano, kusikilizwa wala utetezi; Uwajibikaji kwa makosa ya watendaji walio chini yako.
Hiyo ndiyo demokrasi.

Wabunge wengi wametoa mifano mingi hapa ukiwemo wa Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi, alipokuwa Waziri wa Mambo ya ndani; aliwajibika kwa makosa ya askari huko Shinyanga wakati yeye alikuwa DSM; hatukumsikia akidai apewe nafasi ya kusikilizwa na hata kama angepewa bado angewajibika yeye mwenyewe.

Mheshimiwa Spika, kamati teule inatamka ukurasa wa 37 wa taarifa yake kuwa Ushiriki wa karibu wa Waziri Mkuu katika kila hatua ya zabuni ya umeme wa dharura si lazima uwe ushahidi wa kwamba, kiongozi huyo wa Kitaifa alihusika katika kuibeba Richmond. Unaweza pia ukawa ushahidi wa style yake ya kawaida kabisa ya Waziri Mkuu katika kufuatilia masuala yote ya Kitaifa kwa karibu sana, tukizingatia kwamba, Nchi wakati huo ilikuwa katika kipindi kigumu sana cha ukosefu wa umeme………………." (Mwisho wa Kunukuu)

Hivyo basi ni wazi kwamba Mwakyembe alimsafisha Lowassa kwamba makosa yake hayakuangukia kwenye Sura ya kwanza ya Uwajibikaji wa kiongozi kuwajibika kwa makosa yake mwenyewe. Sura hii ndiyo unayoweza hata ukamwita mtu fisadi. Lakini Lowassa aliwajibika kwa makosa ya watendaji walio chini yake kama alivyoeleza vizuri kabisa Dkt. Mwakyembe.

Anayewajibika kwa aina hii ya pili huwezi kumwita fisadi. Akisifu aina hii ya Edward Lowassa kuwajibika, Dkt. Mwakyembe alisema "……..….. Kitendo cha kuwajibika kwa aina hii, kunaijengea Serikali au taasisi heshima na imani ya pekee katika jamii, na kunatoa picha ya kwamba uongozi unajali na unalielewa tatizo kwa kubeba lawama wao wenywe(Makofi)" Mwakyembe anakwenda mbali zaidi na kuhusisha uwajibikaji huu wa Lowassa na ule wa Mzee Ali Hassan Mwinyi.

SASA BASI; katika hali ya kawaida na kwa kuzingatia hoja hiyo na kauli ya Mwakyembe kama Mwenyekiti wa Kamati Teule na vile vile kwa kutazama namna ambavyo baadhi wa Watu hasa baadhi wa Vijana wenye njaa wanvyotumika kumshambulia EL ni lazma ifikie mahali kama Watanzania wenye kuheshimu utu wa mtu na wenye maadili katika Taifa hili tuulizane Je kuna mengine dhidi ya EL ama ni wivu wa kisiasa kama ambavyo yeye mwenyewe alikwisha sema kuwa tatizo ni Uwaziri Mkuu???

Mwisho tukija kwenye swala la Ufisadi hili halihataji watu kuzungumza sana bali ni kurejea ile list of Shame ya Dk. Slaa pale Mwembeyanga watu walikuwa 11 leo iweje watu wamtazame EL peke yake??

UGONJWA Katika hili wala sitakuwa na mengi ya kuelezea ila wayasemayo haya wala hawatoki CHADEMA, ama CUF au NCCR Mageuzi wako huko huko CCM. Sasa kuna mambo lazma hawa watu wajue;Moja Ugonjwa wa mtu ni yeye na Mungu wake na zaidi labda yeye na Daktari wake. Mgonjwa anayefanya jogging 10Kms every morning?? Mnachekesha kweli.

Lakini la Pili WanaCCM ni lazma na mimi mnijibu hili, ni nani aliyemzima huko CCM wa kumnyooshea Lowassa kidole??
Wengine hudondoka, wengine wanabanduka ngozi, wengine kila dakika wako na vitambaa vya kupangusa jasho hata kama AC iko juu kiasi gani. JK alisingiziwa kama haya lakini leo yuko fiti balaa na anamaliza miaka yake 10 na maneno yenu.

Lakini mtoto wa Mkulima ni nani asiyejua anavyozushiwa kuumwa kila leo lakini nani anayeweza kuthibitisha??
Kama kuna alilopanga Mungu pigeni goti mumwombe alitengua na mjue kuwa Mungu halipi baya kwa baya bali baya kwa jema na jema kwa jema la sivyo Mtaendelea Kusugua Gaga mwenzenu akichanja Mbuga na Nashukuru Mungu EL mnafahamu vizuri na kwake yeye Visasi ni juu ya Mungu na si Binadamu.

Yatosha kusema kule Ikulu watu hawaendi kupasua kuni wala kufetua matofali na mkitaka rudisheni kumbukumbu zenu nyuma Mwai Kibaki aliapishwa kwenye wheel chair, Mzee Mkapa kuna Wakati alitembelea fimbo mpaka anastaafu.. Na wengine wengi.
Manake hoja ilikuwa atakatwa jina sasa imeyeyuka mmekuja na hoja zingine nyepesi mno na bahati mbaya sana mnachodhihirisha mlio wengi ni kwamba hamna mgombea mnaye mwamini mwenye uwezo wa kushindana na huyu Bwana kila leo mnahama kambi. We mgombea unaomba eti wasanii waje siku moja na sinema inasema I Love (Jina lako) hivi kweli??

Lowassa mmempiga stop bado kakaa kimya mnamtukana kila leo bado kakaa kimya mmesingizia mengi bado kakaa kimya lakini ukimya wake majibu yake mnayapata kutoka kwa Wananchi. Nashukuru Wakuu wa Mikoa chini ya Mwenyekiti wao Abbas Kandoro kwa kumweleza Rais ukweli kwamba Mdimu hauziki sasa mbadala kaja Bwana Mizengo Kayanza hivi kweli jamani??

Escrow ndo hiyo ishaanza kumtafuna, Bunge la Katiba nalo analo, Sakata la wale Mawaziri waliojiuzulu aliponea chupu chupu, Kuna hii kitu inaitwa BRN kama Waziri Mkuu pa tulipo leo nini cha kujivunia kwa hilo, mpaka haaSakata la Albino aliweka Historia si Bungeni tu bali Taifa zima…………

Maamuzi ya Taifa hili kwa hapa tulipo lazma kuwe na mtu mwenye kuweza kufanya maamuzi magumu na si kufanya tu na kuwa tayari kuyasimamia na Watanzania waone matunda yatoka nayo na uwamuzi huo.
Namnukuu Freeman Aikael Mbowe "Umasikini si jambo la kujivunia eti utumike kama sababu ya kupata kiongozi kisa ni maskini ama ni mtoto wa mkulima NO…… Watanzania lazma wapinge na kukataa hayo manake huko ni kudumazwa na kujengewa element kwamba umasikini ni sifa"
 
Umejitahidi kumsafisha ndugu yangu Lowassa lakini naona bado. Ni kama kuchota maji baharini ndoo moja utegemee bahari ikauke.
Kuhusu masuala ya afya,jamaa yupo fiti vibaya,muda mwingi tunapishana hapa msasani nyuma ya hostels za chole akiwa jogging. Hata hivyo suala la afya ya mtu binafsi halinihusu mpaka pale mtu huyo atakapokuwa raisi,ndipo suala hilo litakaponihusu (rejea katiba ya sasa sura ya pili).
Unamteteaje tena baada ya hiyo saga alivyoitwa Dodoma mbele ya viongozi wa juu wa ccm, namnukuu,......"Ni kitu gani nilichokuwa nafanya kuhusu Richmond wewe Kikwete usichokijua?" Mwisho wa nukuu.
Ina maana dili lilikuwa akihusika moja kwa moja tena yeye na "first citizen " wa nchi kwa sasa,na si kwamba aliwajibika kwa sababu ya makosa ya subordinates. UNAYAFAHAMU HAYA AU UMELISHWA MANENO YA KUWAHADAA WATANZANIA?
HAPO UNAMTETEAJE?
 
Napata shida sana na hawa spin doctors eti EL ni msafi na healthy! Mm nasema laana ya EL kukosa uongozi ilitoka kwa mtumishi wa mungu Mwl Julius Nyerere, nilikuwa kwenye viunga vya Dodoma May - July 1995 na kwa wakati huo EL alituhumiwa kwa kuwa na mali lukuki zisizo shabihiana na utumishi wake kwa umma, alijeeleza mbele ya kmt kuu, akidai alipokuwa Mkurugenzi AICC alianza kufuga na utajiri wake umetokana na hao ng'ombe lakini Mwl alimwengua kwa kura ya veto kwamba ile tu kuhisiwa ana mali chafu hafai kuingia ikulu, na mimi kama kuna mahali pa kuthibitisha utakatifu wa Mwl ni kwa EL, mwl ni mpakwa mafuta alichofungia duniani na mbinguni kimefungwa, ogopa sana maapizo ya anointed
 
kept it up. tuwe makini tuelewe siasa inayochezwa, uchafu wote wanaubeba hamna msafi walio wasafi hawawezi kuongoza labda tumpe mbatia
 
Una maono ya kweli kabisa,wasiompenda huyu jamaa watajibeba.
 
Timu ya Lowasa sasa ni dhahiri inaishiwa pumzi. Wanatumia muda mwingi kumsafisha badala ya kumnadi. Mwandishi wa mada hii unaona kabisa jinsi anavyotokwa jasho la pua kwa kujaribu kumsafisha. Too bad kwamba uchafu wa Lowasa hausafishiki kamwe hata kama timu yake ikajaza server yote ya JF. Ngumu. Ningemshauri Lowasa aanzishe Chama chake au ajiunge na Chama kingine kama anadhani kuna anakofaa.
 
Tusubiri muda bado upon. Mengi tutayasikia. Naweza kusema kuhusu Mzee Lowassa no kwamba watanzania wanamhitaji sana. Waliomzushia ufisadi Wa Richmond mbona hawakutoa maoni ya kwenye mkutano Wa chama? Huh mchezo ulichezwa na watu wengi kumchafua Edward ila ukweli utajulukana tu. Huyu bwana amekaa nje ya serikali mwaka Wa 8 huu, lakini bado anao ushawishi mkubwa sana kwenye chama na nje ya chama na mvuto mkubwa Kwa wananchi.

Kuhusu hili la ugonjwa rejea gazeti LA mwanachi tah 13.9.2014 ukurasa Wa nyuma Mzee Edward anaonekana yuko fiti. Tumepewa mifano kadhaa Kibaki, lakini hapa kwetu watulimbeza A.Mrema ni mgonjwa lakini kati ya wabunge waliosimamia miradi ya maendeleo katika jumbo lake huwezi kumsahau Mrema. Tuache kuzushiana mabaya. Uhai Wa binadamu uko mikononi mwa Mungu. Wanaojidhani wamesimama waangalie wasije wakawa Wa kwanza kudondoka chini.
 
kwanza la ufisadi wa jamaa utajulikana.najua kamati itakapo kaa kumpitisha mgombea kila upande mara team nan tutajua team zote zinahamasa gan kwa siasa za nchi hii. kuna uwezekano mfumo chama tawala utasitishwa kwa muda, huu ni ukwel sita si aina ya viongozi wazuri ila ukisema mwanaharakati sawa na sifa yake kubwa ni kukosoa ili kurekebisha utendaji wa viogozi. sorry . sina team ila sauti inayopingwa ndipo ukwel ulipo, chambueni mambo tUyaelewe wasitupelekepeleke
 
Lowasa ashakuwa ...........Apsoni kampotosha kabisa.
 
Back
Top Bottom