HABARI ZA ASUBUHI WADAU WOTE WA JAMIIFORUMS
Mimi kama Mtanzania mzalendo naomba niwasilishe malalamiko na kilio cha wanajeshi wetu walioko mstari wa mbele wakihatarisha maisha yao huko JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA WATU WA KONGO wakipambana dhidi ya makundi mbalimbali ya WAASI.
Hivi karibuni JWTZ waliwatuma baadhi ya Wanadhimu toka makao makuu ya jeshi kwenda kuwatembelea na kuwajulia hali makamanda wetu huko KONGO. Katika kufanya hivyo makamanda wetu wakaulizia kuhusu haki zao na maslahi yao kwa uwepo wao huko KONGO, hapo ndipo mgogoro na utata ulipo anzia.
KABLA SIJAENDELEA NAOMBA NITOE UFAFANUZI KIDOGO
UMOJA WA MATAIFA (UN) una chapter mbili katika suala la ulinzi wa amani duniani, CHAPTER SIX na SEVEN. CHAPTER SIX inahusu ulinzi wa amani bila kutumia nguvu kama ilivyo dafur na sehemu nyingine mbalimbali duniani. na CHAPTER SEVEN ni kulazimisha amani kwa kutumia nguvu kama ilivyo huko KONGO ambapo makamanda wetu wanashiriki.
Kila chapter ina malipo yake kulingana na ugumu wa jukumu na hatari wanazokumbana nazo walinda amani. Sasa kuna dhuluma makamanda wetu wanataka kufanyiwa kuhusu malipo yao. Kuna wezi wa mchana wanataka kuwalipa makamanda wetu kwa mujibu wa mkataba wa CHAPTER SIX kitu ambacho sio haki na dhuluma. Stahiki zao zinatokana na CHAPTER SEVEN. Wameona kazi nzito imekwisha ambayo imegharimu UHAI wabaadhi ya makamanda wetu, leo hiii wanataka kuwadhulumu haki zao ilhali wamefanya na wanaendelea kufanya kazi kwa mujibu wa CHAPTER SEVEN.
Mheshimiwa RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, Ndugu, J.M. Kikwete wakati anawaaga na kuwakabidhi bendera ya nchi yetu, aliwatangazia kwamba makamanda wetu watafanya kazi chini ya CHAPTER SEVEN na akaliambia bunge hivyo hivyo iweje leo malipo yawe ni ya CHAPTER SIX?Je Raisi alidanganya?
OMBI LANGU
Ninaomba MHESHIMIWA RAISI kama hizi misheni za kulinda amani hazina faida na makamanda wetu, usizikubali na BUNGE vilevile lifuatilie maslahi ya makamanda wetu kwani wanaofaidika ni baadhi ya vigogo jeshini na serikalini. Hii sio haki, wanaomwaga damu zao wanazidi kuwa maskini kila kukicha ilhali wanyonyaji wachache wakijitajirisha kupitia damu za makamanda wetu.
Pia nawaomba wadau wengine ambao mnaweza kulisimamia hili suala kama vile WABUNGE, WANASIASA na yeyote Yule atakayeguswa, please lindeni haki zao hawa makamanda wetu.
UWEZO WANGU NI MDOGO SANA LAKINI SILAHA YANGU NI KALAMU YANGU( Niko tayari kukosolewa kwa mapungufu yoyote utakayo yaona)
NB: Please MODS msiufute uzi huu ili usomwe na wengi na haki ipatikane kwa wanajeshi wetu walioko mstari wa mbele kwa wale watakao weza kuwasaidia