Ufisadi bilioni 5.7 wazuiwa Kinondoni

Ufisadi bilioni 5.7 wazuiwa Kinondoni

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,538
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (pichani) ameamuru kusitishwa mara moja malipo yanayofanywa kwa makandarasi waliojenga barabara tano za ndani ya wilaya hiyo.

Amefanya hivyo kwa maelezo kuwa watendaji wa Manispaa hiyo, wameshirikiana na makandarasi hao kuiibia serikali Sh bilioni 5.7. Fedha hizo ni ongezeko ambalo makandarasi hao, wanatakiwa kulipwa baada ya kujenga barabara hizo, ambazo thamani halisi ya ujenzi huo ni Sh bilioni tano.

Lakini, katika hali isiyo ya kawaida, makandarasi hao wanatakiwa kulipwa Sh bilioni 10, ongezeko ambalo ni zaidi ya asilimia 100. Akizungumza jana Dar es Salaam, Makonda alisema taratibu za Serikali zinataka kama barabara haikukamilika ndani ya muda uliowekwa kwa sababu mbalimbali, ikiwemo mvua na sababu zinginezo, mkandarasi anatakiwa kulipwa fedha zaidi ambazo ni asilimia 15 ya thamani ya fedha za mradi.

"Lakini kinachostaajabisha katika miradi hii ya barabara, fedha ambazo zimeongezeka ni zaidi ya asilimia 15, kiasi hiki ni zaidi pia ya asilimia 100, wametumia utaratibu gani kulipa fedha hizi za ziada kwa makandarasi hawa?" Alihoji Makonda.

Alizitaja barabara ambazo watendaji wamezitumia kufisadi fedha za umma kuwa ni ujenzi wa barabara ya Lion kwa kiwango cha lami yenye thamani ya Sh milioni 592.1, lakini nyongeza ya fedha zilizoongezeka ni Sh milioni 860.1 na hivyo kufanya mradi huo kugharimu Sh bilioni 1.4.

Barabara ya kutoka Biafra hadi Embassy, matengenezo yalikuwa ni Sh milioni 507.9 na fedha zilizoongezeka ni Sh milioni 487.5 jumla ya malipo kwa mkandarasi ni Sh milioni 994, barabara ya Mabatini thamani ya mradi ilikuwa Sh milioni 655.5 na fedha zilizoongezeka ni Sh milioni 777.8 na jumla ya mradi kugharimu Sh bilioni 1.4.

Makonda alitaja barabara nyingine zilizojengwa kwa kiwango cha lami zenye ufisadi ni ya Journalism, ambayo ujenzi wake ulikuwa ugharimu Sh bilioni mbili, nyongeza ya fedha katika mradi huo ni Sh bilioni 1.8 na hiyo kufanya mradi huo hugharimu Sh bilioni 3.8, Barabara ya Maandazi ambayo thamani ya mradi ni Sh milioni 799 imeongezwa kiasi cha fedha Sh bilioni 1.2 na hivyo kufanya mradi wote kugharimu Sh bilioni 2.

"Nyongeza hizi zinatia shaka na ni jambo la kushangaza, nimeamuru makandarasi wasiendelee kulipwa fedha hizi na nimetoa siku tano kwa ofisi ya uchunguzi ya mkoa ichunguze malipo haya na mafaili ya miradi hiyo yaletwe ofisini kwangu mara moja," alisema Makonda.

Alisema ili malipo ya ziada yalipwe, lazima Bodi ya Zabuni ya Wilaya na Bodi ya Mfuko wa Barabara, ziidhinishe malipo hayo. "Lakini cha kushangaza katika malipo haya, yanayoendelea kufanywa na Manispaa, makandarasi wamelipwa kabla hata bodi hazijatoa ukubali wa malipo haya kufanyika," alisema.

Alisema Bodi ya Mfuko wa Barabara katika ripoti yao, walikataa fedha hizo za malipo ya zaida zisitolewe. Lakini, alisema fedha hizo zilitolewa na Manispaa kwa makandarasi hao na hiyo inaonesha kwamba kuna mchezo mchafu, umefanywa kati ya watumishi wa Manispaa na makarandasi wenyewe.

Alisema wahusika wakuu katika malipo hayo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa, Kitengo cha Manunuzi, Mhandisi wa Barabara wa Manispaa ambao ndio wanatakiwa kutoa maelezo ya kuwepo kwa nyongeza hiyo ya malipo kinyume cha taratibu za Serikali.

"Watu wanadai naingilia kazi za watu, nisipobaini uozo huu kwenye wilaya yangu sifai kuwa mkuu wa wilaya, haiwezekani watu wafisadi fedha za umma kiasi hiki wakati tunakosa hata pesa ya kujenga wodi ya wazazi pale Hospitali ya Mwananyamala," alisema Makonda.

Alisema ataendelea kupambana, kuhakikisha kwamba kila mwananchi anafaidika na keki ya Serikali ;na sio watu wachache ambao wamepewa dhamana ya kufanya kazi kwenye ofisi za umma wafaidike na keki hiyo.

Barabara hizo ni nje ya barabara zingine, ambazo Makonda mwanzoni mwa mwaka huu aliziundia tume kuchunguza ujenzi wake, ambao walidai ulikuwa chini ya kiwango hali inayofanya mvua zikinyesha barabara hizo zinageuka mahandaki.

Tume hiyo ilibaini ujenzi kuwa chini ya kiwango, lakini mabilioni ya fedha zimetumika katika ujenzi huo. Ilipendekeza hatua kuchukuliwa kwa wahusika waliohusika kujenga barabara hizo, ambazo mvua ikinyesha zinageuka mashimo.

Chanzo: Habari Leo
 
Hivi kipindi cha utawala wa Kikwete, nchi hii ilikuwa na sheria na vyombo vya dola au vilikuwa likizo? napendekeza upelekwe mswada bungeni kurekebisha sheria ya kuwaondolea kinga marais wastaafu kinga ya kushtakiwa. Kwa kuwa kila rais asiye na mapenzi mema na nchi hii ataingia madarakani na kuhujumu nchi kisha anastaafu akijua kabisa pamoja na ubadhirifu wote alioufanya hatashtakiwa. Marais wote walioongoza nchi nchi baada ya Nyerere, yaani Mwinyi, Mkapa na Kikwete na wafuasi wao wote hawa wanastahili kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa hujuma walizolifanyia taifa. Hatuwezi kufuga ujinga huu uendelee milele na milele huku nchi ikiendelea kuangamizwa na marais uchwara ambao hawana uzalendo na taifa lao.
 
Hivi na hilo ni gazeti
 
Hapa dogo nampongeza hatakama anaingilia mambo yasiyomhusu lakin yana maslahi kwa taifa.
 
Tatizo in LA wabunge wetu pamoja na wanasheria wa nchi hii kuzifumbia macho vipengele vya katiba visivyo na maslahi na nchi. Sijui kwanini hawataki kuibadili katiba ili kila mwenye kufanya kosa awajibishwe kwa mujibu wa sheria za nchi. Tuige mfano wa nchi ya misri juu ya kushtakiwa marais kwa ufisadi.
 
HONGERA DC MAKONDA kwa uthubutu wako juu ya swala hili na huo ni wizi mweupe
 
Tatizo in LA wabunge wetu pamoja na wanasheria wa nchi hii kuzifumbia macho vipengele vya katiba visivyo na maslahi na nchi. Sijui kwanini hawataki kuibadili katiba ili kila mwenye kufanya kosa awajibishwe kwa mujibu wa sheria za nchi. Tuige mfano wa nchi ya misri juu ya kushtakiwa marais kwa ufisadi.

Wao katiba wanazoshughulikia na kususia ni zile zitazowapatia madaraka, mengine hawaoni.
 
Hivi kipindi cha utawala wa Kikwete, nchi hii ilikuwa na sheria na vyombo vya dola au vilikuwa likizo? napendekeza upelekwe mswada bungeni kurekebisha sheria ya kuwaondolea kinga marais wastaafu kinga ya kushtakiwa. Kwa kuwa kila rais asiye na mapenzi mema na nchi hii ataingia madarakani na kuhujumu nchi kisha anastaafu akijua kabisa pamoja na ubadhirifu wote alioufanya hatashtakiwa. Marais wote walioongoza nchi nchi baada ya Nyerere, yaani Mwinyi, Mkapa na Kikwete na wafuasi wao wote hawa wanastahili kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa hujuma walizolifanyia taifa. Hatuwezi kufuga ujinga huu uendelee milele na milele huku nchi ikiendelea kuangamizwa na marais uchwara ambao hawana uzalendo na taifa lao.

Sioni sababu ya kumfungulia mashtaka Rais tu hapa ilibid tuanze na wale waliothibitisha kwa ndimi zao wenyewe kwamba hawakufanya kazi katik vipind walivopewa nyadhifa za kufanya kazi na serikali waliyoitumikia.

Kipind cha kampeni tumeshuhudia waziri mkuu mstaafu akikiri kwa kinywa chake mwenyewe kwamba serikali ya ccm ktk kipind cha miaka hamsini haijafanya chochote na imeishiwa pumzi. Nadhani tuanze na huyu kumuuliza alikua anafanya nn alipokua pale kabla hatujaenda kwa rais maana sheria zinaruhusu kwa huyu Waziri mkuu mstaafu. Anakula pension zetu bure tuwashawish wBunge warekebishe sheria kutengua pension za mawaziri wakuu wastaaf wasipewe chochote kwa kuwa hawakufanya kazi iliyopaswa kufanywa wakati huo.

Shame on him aiseeee
 
jamen barabara ya mabatini imejengwa lini mbona ni mahandaki?leo nimepasua shock up pale,,,mbona machozi yananitoka kwa mambo haya,,,,barabara ya Biafra si wameachia kule bondeni hawajafikia mpka barabara ya kinondoni,,,,kwani hazikaguliwi hizi barabara kabla ya malipo?
 
Back
Top Bottom