Christian Jacob,naibu mwenyekiti wa chama cha Republican cha mrengo wa kulia amesema kuwa rais Emmanuel Macron amepoteza heshima na uaminifu kutoka kwa wananchi na hivyo uchaguzi mpya unapashwa kuandaliwa nchini Ufaransa.
Jacob amekua akikosoa sera za Macron tangu alipoingia madarakani.
"Macron alisema analenga kufanya mabadiliko makubwa, lakini nchi imekuwa katika hali mbaya", alisema Jacob akisisitiza kuwa rais huyo amepoteza heshima na imani ya Wafaransa.
Jacob ameongeza kwa kusema kuwa uchaguzi ni njia pekee ya kuonyesha uhalali wa rais na serikali, hivyo amesisitiza haja ya kuandaa uchaguzi mpya wa urais.