Ufafanuzi: Kwanini bei ya hisa za vodacom ni shilingi 850/=?

Sudysoko

JF-Expert Member
Aug 19, 2015
449
180
Watu wengi wana maswali ya ziada ni kwanini Bei ya hisa za Vodacom ni Shilingi 850 kwa kila hisa?

Bei hii ya hisa ilifikiwa baada ya wakurugenzi wa Vodacom kuafikiana pamoja na mshauri mkuu kwa kuangalia baadhi ya mambo kadhaa mfano;

•Muonekano na Mwelekeo wa uchumi wa Tanzania.

•Utendaji wa kifedha wa kampuni pamoja na matarajio ya kampuni.

•Ulinganifu wa thamani za hisa za kampuni zinazofana na kampuni ya Vodacom kwenye masoko ya hisa ya Bara la Afrika kabla ya kuwekwa kwa bei kamili ya kila thamani ya hisa moja.

•Matarajio ya mtiririko wa fedha wa kampuni hiyo kwa lugha ya kiuchumi tunasema (Discounted Cash Flow)
Tathmini ya kampuni imeangalia kwa kiasi hali ya kina ya kibiashara yakampuni ambapo Wakurugenzi wenyewe wanaamini ilihusisha utendaji wa hivi karibuni, na rasilimali ambazo kampuni ya Vodacom imewekeza kuwa itawezekana kabisa kuyafikia malengo.

Vile vile zipo njia kadhaa za kutathmini (Valuation Methodologies) katika kufikia hitimisho hili la bei.

Njia hizo ni pamoja na kufanya ulinganifu (comparative analysis) na kampuni nyingine za mawasiliano katika Bara la Afrika, kwa ukaribu zaidi nchi kama Kenya na Afrika ya Kusini, kutokana hapa nyumbani (Tanzania) hakuna kampuni inayofanana na Vodacom ambayo imeorodhesha hisa zake sokoni.

Katika kufanya ulinganifu huo, kampuni huzingatia kufanya marekebisho ya tathmini kwa kuangalia mambo kama utofauti wa ukubwa wa Soko, Idadi ya watu na tofauti za kiuchumi (Kifedha)

Baada tathimini hatua iliyofuata ili kupata bei kamili unafanyika mchanganuo wa uhusiano (Regression Analysis) siku zote ni kati ya ukuaji wa mapato na viashiria vya biashara ili kuweza kupata thamani za hisa.

Kwa kutumia njia ya Discounted Cash Flow analysis unaweza kupata matokeo ya tathmini yanayoendana na ulinganifu wa makampuni kwa njia ya viashiria vya kibiashara .

Mwisho thamani ya jumla ya wanahisa inayopatikana kwenye tathmini hugawanywa kwa idadi ya hisa zote na kupata thamani ya kila hisa ndiyo sababu kila Hisa moja ya Vodacom inauzwa kwa shilingi 850.

Natumaini nimeeleweka hapo!
[HASHTAG]#WekezaNaVodacom[/HASHTAG]
[HASHTAG]#PowerToYou[/HASHTAG]
vodacom.jpg
 
Hamna kitu kinanichanganya kama ninavosikia neno kununua hisa..yani ni nini faida yake...mfano mimi nikinunua hizo hisa 100 kwa 85000 napata faida gani...na je kina uwezekano wa kupata hasara pia.na hasara au hizi faida inatoka au inapatikana vipi
 
Haha
 
Kwa kifupi tu...kama ukinunua hisa kwa mia nane...then baada ya muda zikapanda thamani mpaka 1000!! Ukiuza kwa bei ya soko yaani 1000 utapata 200 faida kwa kila hisa!! Mfano kama ulinunua hisa 100 kwa 85000 basi zikipanda bei na kuwa 1000 kwa hisa ukiuza zote utapata laki moja!!

Like wise zikishuka bei thaman pia inashuka na utapata hasara!!

Cc figganigga
 
Bado sijaelewa...kidogo.
Hizo hisa ni kitu unaweza shika,?
Ni mikataba flan?
Au ni nini
 
Kwa kifupi tu...kama ukinunua hisa kwa mia nane...then baada ya muda zikapanda thamani mpaka 1000!! Ukiuza kwa bei ya soko yaani 1000 utapata 200 faida kwa kila hisa!! Mfano kama ulinunua hisa 100 kwa 85000 basi zikipanda bei na kuwa 1000 kwa hisa ukiuza zote utapata laki moja!!

Like wise zikishuka bei thaman pia inashuka na utapata hasara!!

Cc figganigga

bei utakayouza 1000
itakuwa na thamani sawa na sasa 850.

thamani ya pesa ya leo sio sawa na ya kesho.
 
Kwakweli ktk vitu ambavyo ni giza totoro kichwani mwangu ni hili neno HISA na maana zake. Asanteni
 
Kwa kifupi, unaponunua hisa, unakua mmiliki wa hiyo kampuni. Inamaana wakipata faida, unagawiwa faida kutokana na idadi au wingi wa hisa zako. Hali kadhalika wakipata hasara, itakugusa kwa sababu bei ya hisa itashuka.
 
Ni vizuri kuwekeza pesa ambazo hauzihitaji kuzitumia hivi karibuni. Hisa ni uwekezaji wa muda mrefu na unakua na tija ukinunua hisa nyingi. Hata hivyo ni vizuri kupata ushauri wa kitaalam kabla ya kufanya maamuzi ya kununua hisa.
 
Back
Top Bottom