Udugu wa muungano

mpemba mbishi

JF-Expert Member
Nov 27, 2011
1,132
185
Ngoma yataka matao unapotaka kucheza, Na ujuzi uwe nao kucheza si kufyekeza, Uchungu nilionao Leo nataka eleza.
UDUGU TULIONAO WENZETU MWATUUMIZA! Natohoa ya ukweli japo si uwanja wangu, Yanatuumiza kweli tumejawa na uchungu,
Twatafutana muhali tutaupiga mafungu UDUGU TULIONAO WENZETU
MWATUUMIZA! Wale walouasisi kutaka mafanikiyo ila wenzetu mafisi hale lenu kusudio, mwatugombanisha sisi furaha yenu ya moyo.
UDUGU TULIONAO WENYETU
MWATUUMIZA! Tena mwatung'ang'aniza faida mwapata nyinyi,
wale waliouanza wao wapo kaburini, suali twajiuliza; nini lekua dhumuni?
UDUGU TULIONAO WENZETU
MWATUUMIZA! Tulishasema ni koti wenzetu
hamukujua, hivi sasa ni wakati tunataka kulivua, yeli yenu mikakati 'Zenj' yetu kuiua.
UDUGU TULIONAO WENZETU WATUUMIZA! Udugu udugu gani nyinyi kutaka vya kwetu, tena vile vya thamani kuchimba mafuta yetu, vyenu vimo makwapani hatwepata vithubutu. UDUGU TULIONAO WENZETU
MWATUUMIZA! Kila chetu cha thamani sio siri mwakitaka, mpaka vya BAHARINI Alivyotupa Rabbuka, kama sio UKOLONI Vipi mutautamka,
UDUGU TULIONAO WENZETU MWATUUMIZA! Sasa tunasema basi tumechoka miyeyusho, turadhi na tule nyasi ila mwaka huu mwisho, hebu tupeni nafasi hakuna kisicho MWISHO. UDUGU TULIONAO WENZETU
MWATUUMIZA!
 
Fanyeni kazi kwa bidii..chagueni viongozi bora na kuwasimamia mtapata maendeleo..Kushindwa kwenu kuendelea hakusababishwi na huu muungano.Hata huku bara tuna matatizo chungu nzima na hayaishi leo, kwani mmeyasababisha ninyi.

Kenya nao wana matatizo yao chungu nzima nayo yamesababishwa na Muungano?
 
Back
Top Bottom